Madhumuni ya Sera ya Faragha

Ufuatao ni muongozo wa kupata taarifa na kuzichambua kwa lengo la kutumia tovuti.

 Matumizi ya Taarifa za mteja.

Taarifa za mteja (inamanisha kwamba taarifa zote zinazo kuhusu kama vile kitambulisho, Jina lako, namba ya simu au barua pepe, anwani ambazo zinajulikana katika sera hii ya faragha kama ‘ Taarifa zako’) itashughulikiwa na Parimatch (ambayo ni pamoja na wakala na wafanyakazi) na (sahihi) washirika wetu na wasaidizi wakuu ili kuweza kutoa huduma kamili kwa wateja. Taarifa za mteja zinachukuliwa wakati anafanya usajili wa kupata akaunti ya Parimatch; au mteja anapowasilisha tatizo Parimatch.

Kwa kutumia huduma yoyote, mteja unapaswa kusoma na kukubaliana na masharti ya sera ya faragha na kwamba mteja hutupatia taarifa zake (ili kuzuia wasiwasi, kwa kutumia maoni katika tovuti moja kwa moja au pindi mteja anapokamilisha mchakato wa usajili wa akaunti yake)

Je! ni aina gani za taarifa ambazo mnachukua na kuzitumia

Parimatch inachukua taarifa za mteja ili:

Kumuwezesha mteja kufungua akaunti yake na aweze kutumia kikamilifu huduma zote zinazotolewa pamoja na kuweka beti na kucheza.

Kutuwezesha sisi kupokeaa maswali na maoni kutoka kwa mteja ambapo nasi tutamjibu kupitia kitengo chetu cha huduma kwa wateja kumjibu mtandaoni

Zingatia kanuni zinazofaa kuhusu usajili wa mteja, kwa mfano kukamilisha uhakiki wa umri; na kumjulisha mteja juu ya matukio ya baadaye, ofa na promosheni kutoka Parimatch.

Mbali na madhumuni mapana yaliyoainishwa katika aya ya 1 hapo juu, Parimatch itatumia taarifa za mchezaji tu, pamoja na kushirikiana na washirika wengine katika kuzichakata taarifa hizo ambao huziifadhi (pamoja na taarifa sahihi za mteja) kwa niaba yetu kwa:

  • kuanzisha, kufanya kazi na kusimamia Akaunti ya mteja;
  • kutoa huduma yoyote ambayo imeombwa kwetu, na kwa kusudi lolote linalofaa linalohusiana na utoaji huo;
  • Kudhibitisha usahihi wa taarifa za mteja, pamoja na kuficha baadhi ya taarifa kwa washirika wetu (zikiwemo taarifa za kifedha, uthibitisho wa umri) kuhusiana na malengo kama haya (rekodi ya utaftaji utabaki na washirika wetu ambapo ataweza kutumia taarifa hiyo kusaidia kampuni zingine kwa madhumuni ya uthibitishaji);
  • kuandaa takwimu zinazohusiana na utumiaji wa huduma na kwako na wateja wengine;
  • kuandaa na kuonyesha masoko yote yanayofaa kwa mtu mmoja mmoja
  • Kuwatumia ujumbe wamiliki wa akaunt juu ya kuwataarifu mabadiliko ya huduma, maboresho na mabadiliko ya sheria (ambayo yanahusiana na sera ya faragha).
  • kufuata matakwa ya kisheria au kufuata taratibu za kisheria au kulinda masilahi ya mteja au mtu mwingine.
  • Uchunguzi wa tuhuma zisizo halali, za ulaghai au shughuli zingine zisizo sawa zilizounganishwa na Huduma;
  • kuripoti kwa uhalifu au uhalifu unaoshukiwa, pamoja na utapeli wa pesa mtandaoni au udanganyifu wowote;
  • Dhumuni jingine jingine lolote ambalo ni muhimu kwa utekelezaji wa majukumu yetu ya makubaliano kwa mteja.

Parimatch haitoweza kutuma taarifa za mteja zilizotolewa kwa mtu mwingine kwa madhumuni ya kibiashara ay matangazo.

Parimatch inaweza kutumia jina la ukoo la mteja au / jina la kwanza na mkoa kwa matangazo

Simu zote kutoka kwa wateja zitarekodiwa na kitengo cha huduma ya Parimatch kwa lengo la usalama na uboreshaji wa huduma.

Tunaweza kuhamisha taarifa za mteja iwapo tutahamisha au kuuza biashara yetu au sehemu yoyote ile; pamoja na tukio la ufilisi.

Ikiwa mteja hatotaka kutumiwa taarifa zake kulingana na madhumuni ya hapo juu anaweza kuwasiliana nasi ili kuweza kuzuia..

Kuboresha taarifa za mteja.

Mteja anaweza kuboresha au kufuta taarifa zake muda wowote kutoka katika akaunti yake ya Parimatch kupitia 'Akaunti yangu / Boresha taarifa ya Akaunti' (inapopatikana); au kwa kuwasiliana na Huduma kwa Wateja.