Wanacheza – Unashinda Jiunge sasa
Mwanzo / / Parimatch inaanza udhamini wa Klabu ya Mbeya City kwa msimu wa 2022-23

Tunapenda kuutaarifu umma kuwa Leo, Jumanne Tar 9 Agosti 2022, tumeingia rasmi makubaliano ya mkataba wa udhamini wa Klabu ya Jiji la Mbeya ‘Mbeya City’, ambayo inashiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika msimu huu wa 2022/2023.

Mkataba huu ni wenye faida kwa pande zote mbili. Mbeya City ni moja ya klabu kubwa kwa hapa Tanzania hususani ukiangalia idadi ya mashabiki na ushawishi katika soka na hiyo ndio sababu tosha ya sisi kurejea tena kufanya udhamini na Mbeya City kwa msimu huu mpya. Wa 2020/2021 tulikuwa wadhamini wakuu kwa mara ya kwanza.

Sisi kama Parimatch Moja ya jukumu letu kubwa ni kuhakikisha michezo inakua kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya kimataifa.

Lakini pia Tunaendelea na michakato mablimbali ya kuunga mkono vilabu vingine kutoka ligi kuu, ligi daraja la kwanza na hata Vilabu Chipukizi. Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za TFF na bodi ya ligi kuhakikisha ligi za Tanzania zinakuwa na tunaenda kimataifa.

Hivyo tumeamua kuunga mkono mbeya city, ili wapenzi wasoka waendelee kupata burudani stahiki.

Pamoja na fedha taslimu (itabakia kuwa bayana kwa pande husika), Parimatch pia itatoa vifaa kwa klabu pamoja na ukarabati mdogo wa uwanja wa Sokoine hasa katika eneo la kukaa la benchi la ufundi kwa awamu ili kuufanya uwanja kuendelea kuwa na sifa ya kuchezewa michezo ya ligi kuu.

***

Parimatch inaendesha shughuli za michezo ya kubashiri mtandaoni na imesajiliwa na bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania kwa takriban miaka 5 sasa. Kimataifa tupo zaidi ya nchi 15 ikiwa na wateja zaidi ya milioni moja duniani kote.

Ndani ya hii miaka mitano tumeendesha programu mbalimbali za kuinua michezo Tanzania kama Amsha ndoto na leo ni hatua nyingine tena tunapiga katika kukuza michezo.

Je, unahitaji kuwa wa kwanza kupata taarifa mbalimbali?

Subscription was successfully completed.