Tarehe 9 Agosti, 2021, New Delhi — PMI, kampuni inayotoa huduma za teknolojia, masoko na mawasiliano kwenye sekta ya kamari na michezo ya kubashiri kwenye masoko ya kimataifa, kama vile Afrika, Asia, Ulaya, na Amerika ya Latini, inafurahia kutanganza makubaliano ya kibiashara na moja ya klabu kubwa na maarufu zaidi barani Ulaya na duniani kote, klabu yenye mafanikio zaidi ya zote nchini Uingereza kwenye miaka ya karibuni itakuwa mshirika wa kibiashara wa Parimatch Tech kwa misimu mitatu ijayo.
Parimatch itatumia ukubwa wa chapa ya Chelsea pamoja na rasilimali zake za kidijitali na kijamii kutengeneza fursa za kujitangaza na kukua kwa chapa zote mbili.
“Utofauti wa kipekee wa Chelsea, ubora, umakini na moyo wa kujituma vinaendana na malengo ya Parimatch ya kukua huku tukizidi kuwaburudisha wateja wetu. Kuingia kwenye ushirika na mabingwa wa Ulaya wa mwaka 2020/2021 ni jambo la kufurahisha na kuheshimisha kwa chapa tunayoiwakalisha duniani kote. Kwa bahati nzuri, PMI ipo kwa ajili ya kufikia malengo makubwa zaidi huku tukikonga nyoyo za wateja wetu, tupo tayari kwa ajili ya miaka mitatu ijayo ya mkataba huu! Kwa kuwa chapa zetu zote mbili zina malengo ya kuzidi kufanikiwa zaidi, sisi PMI tunaamini kuwa ushirika huu utakuwa wa mafanikio kwa pande zote mbili na washirika wetu wengine bila kusahau mashabiki wa soka duniani kote,’’ anasema Anton Rublevskyi, Mkurugenzi Mkuu wa PMI.
“Chelsea na Parimatch kwa pamoja wanatafuta mafanikio makubwa, tupo tayari, tunajiamini na cha muhimu zaidi ni kuwa wote tumezaliwa kushinda, mwaka jana ulikuwa ni mwaka mzuri kwa Parimatch kwani walikua na kuzidi kujitanua na kuingia masoko mengine mapya, huku wakifanyia kazi miradi mikubwa ya kukuza sekta nzima ya michezo ya bahati nasibu, vilevile Chelsea tumezidi kuonesha ubora wetu kwa kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya kwa mara ya pili kwenye historia yetu, tumejiandaa na tupo tayari kwa ushirika huu pamoja na fursa zote utakazozileta,’’ Guy Laurence, Mkurugenzi Mkuu wa Chelsea FC, akizungumzia ushirika huu na Parimatch Tech.
—
Kuhusu PMI
PMI ni kampuni ya huduma inayojihusisha na kuunda na kutengeneza mipango kazi ya ukuaji wa chapa ya Parimatch kwenye masoko ya kimataifa kama Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Latini. Kampuni inatoa huduma za kutengeneza teknolojia, masoko na mawasiliano kwa washirika kwenye sekta ya michezo ya kubashiri na bahati nasibu kiujumla.
Uvumbuzi, teknolojia mpya na nia ya dhati ya kutoa huduma za ubora wa kipekee kwa wateja ndiyo nguzo kuu ya PMI
Kuhusu Klabu ya Soka ya ChelseaÂ
Klabu ya soka ya Chelsea ni moja ya vilabu vikubwa zaidi barani Ulaya na duniani kote baada ya kushinda ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mwaka 2021 kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester City kwenye fainali iliyofanyika jijini Porto.
Klabu imeanzishwa mwaka 1905, Chelsea ni klabu ya soka iliyopo katikati ya jiji la London, uwanja wake wa nyumbani ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji 41,000 ukitambulika kama Stamford Bridge, Jina la utani la klabu ni “The Blues” klabu ilinyanyua komba la ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012 na pia ikiwa imeshinda kombe la ligi kuu ya Uingereza mara tano, kombe la FA mara nane, kombe la ligi mara tano, ligi ya Europa mara mbili na UEFA Super Cup mara moja na kombe la Championship mara moja, mwaka 1955.
Ushindi wa ligi ya mabingwa Ulaya wa mwaka 2021, uliifanya Chelsea kuwa klabu pekee yenye makombe mawili ya UEFA, baada ya kunyakua ligi ya mabingwa, ligi ya Europa, na kushinda kikombe kingine cha washindi wa UEFA.
Chelsea ikiwa na kikosi chenye wachezaji wanaofahamika zaidi duniani, pia imewekeza kwenye timu yao ya vijana kwa kutengeneza akademi ya kipekee na uwanja wa mazoezi bora kabisa unaofahamika kama Cobham, Surrey. Tangu kufunguliwa kwa akademi hiyo, klabu imeshinda makombe saba ya FA ya vijana, kombe la vijana wa UEFA mara mbili mfululizo mwaka 2015 na 2016, na kombe la ligi kuu chini ya miaka 18 mwaka 2017 na 2018.
TImu ya wanawake ya Chelsea pia imesaidia kupata mafanikio kibao kwa kushinda mashindano ya Super League ya wanawake kwa mara ya nne mwaka 2021. Vilevile walishinda kombe la wanawake la FA pamoja na ligi mwaka 2015 na 2018, na kunyanyua makombe yote mawili ya Super League ya wanawake mwaka 2020 na mwaka 2021.
Chelsea Foundation pia inajivunia kuwa na msaada mkubwa kwa jamii kwa kusaidia kuboresha maisha ya watoto na vijana duniani kote.