Wanacheza – Unashinda Jiunge sasa
Mwanzo / / Wachezaji 10 Bora wa Kitanzania wa Mpira wa Miguu wa Muda Wote: Kutoka Mbwana Samatta hadi Athuman Idd

Tanzania ni nchi nzuri ya kufikia kwa wengi, lakini mbali na mbuga zake za wanyama za kuvutia na utamaduni motomoto kuna mpira wa miguu wa Kitanzania. Mpira wa miguu ndio mchezo wa kitaifa kwa Tanzania na umekuwepo kwa muda mrefu nchini humo.

Mbali na umaarufu wake, mafanikio katika mashindano ya mpira wa miguu nje ya bara la Afrika daima hayajawahi kuwa rahisi. Ingawa hakujawahi kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa kutoka Tanzania kwenye ngazi za kimataifa, anapotokea mmoja, mara zote huwa anavutia sana.

Kwa heshima ya wachezaji hawa wa zamani na wa sasa, tumetengeneza orodha inayoangazia 10 kati ya wachezaji bora wa mpira wa miguu ambao wamevibariki viwanja miongo ya karibuni.

1. Mbwana Samatta

Mbwana Samatta

Mbwana Samatta ni moja ya wachezaji wa mpira wa miguu wenye kipaji waliowahi kutokea Tanzania. Mzaliwa wa Dar es Salaam, Tanzania, mnamo 1992, Samatta alianza maisha yake ya soka na TP Mazembe huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa haraka alikuja kuwa mtu muhimu kwa timu hii.

Samatta aliwasaidia kushinda mataji kadhaa, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2015. Baada ya kucheza kwa mafanikio TP Mazembe, Samatta alihamia Ubelgiji, ambapo kwa sasa anaichezea Genk kwa mkopo kutoka Fenerbahce.

2. Mwadini Ali

Mwadini Ali

Mwadini Ali ni mchezaji mwingine wa Kitanzania wa mpira wa miguu ambaye kwa mapana anachukuliwa ni moja ya wachezaji bora katika historia ya nchi yake. Mzaliwa wa Dar es Salaam, Tanzania, mwaka 1985, Mwadini alianza kuichezea Azam FC na kuwa sehemu muhimu ya timu yao. Alikuwa muhimu kwenye mafanikio yao katika Ligi Kuu ya Tanzania na aliwasaidia kushinda vikombe vya hapa nyumbani.

3. Hadji Mberwa

Hadji Mberwa anachukuliwa kuwa moja ya wachezaji wa Kitanzania wa mpira wa miguu mwenye umaarufu zaidi. Akiwa ni mzaliwa wa Tabora, Tanzania, mnamo 1980, Mberwa alianza kucheza soka la kulipwa kunako Moro United, baadae akatimkia Rayon Sports na JKT-Ruvu kabla ya kutundika daruga.

4. Said Maulid

Said Maulid

Said Maulid ni mchezaji wa Kitanzania wa mpira wa miguu ambaye amejitengenezea jina katika ulimwengu wa soka. Akiwa ni mzaliwa wa Namageni, Tanzania, mnamo 1984, alianza kusakata kabumbu na Simba SC na baadae kujiunga na Yanga na Onze Bravos. Alijitengeneza kuwa mtu muhimu kwa kila timu aliyoichezea, kumfanya ashinde mataji ya ligi na vikombe vya nyumbani.

5. Shomari Kapombe

Shomari Kapombe

Shomari Kapombe ni moja ya wachezaji wa Kitanzania wenye mafanikio zaidi katika historia. Akizaliwa Morogoro, Tanzania, mwaka 1992, alianza maisha yake ya soka akiichezea Simba na amezichezea Cannes na Simba. Ana mataji 5 ya ligi na vikombe 2 vya nyumbani. Shomari kwa mara ya kwanza aliitwa timu ya Taifa ya Tanzania mwaka 2011.

6. Stephano Mwasika

Stephano Mwasika ni mchezaji wa Kitanzania wa mpira wa miguu anayeheshimika ambaye amejitengenezea jina katika ulimwengu wa soka. Akiwa amezaliwa Mbeya, Tanzania, mnamo 1987, alianza kwa kuichezea Prisons FC na vilabu kadhaa kama Yanga, Moro United, na Ruvu Shooting. Aliitwa mara 18 kwenye timu ya Taifa ya Tanzania.

7. Shadrack Nsajigwa

Shadrack Nsajigwa

Shadrack Nsajigwa ni moja ya wachezaji wa Kitanzania wa mpira wa miguu wenye kipaji na mafanikio kwa muda wote. Akiwa ni mzaliwa wa Dar es Salaam, Tanzania mwaka 1984, alianza kucheza soka la kulipwa klabu ya Prisons FC Mbeya. Aliitwa mara 51 kwenye timu ya Taifa ya Tanzania.

8. Erasto Nyoni

Erasto Nyoni

Erasto Nyoni ni moja ya wachezaji wa Kitanzania wa mpira wa miguu anayesherehekewa sana, akiwa ameyafikia mafanikio makubwa kipindi chake chote cha kucheza soka la kulipwa. Alizaliwa Dar es Salaam, Tanzania, mwaka 1988. Alianza kukipiga kunako Rolling Stone na kwa sasa anaichezea Simba SC. Erasto ameitwa mara 51 kwenye timu ya Taifa ya Tanzania.

9. Haruna Moshi

Haruna Moshi

Haruna Moshi ni mchezaji wa Kitanzania wa mpira wa miguu ambaye amejitengenezea jina kama moja ya wachezaji bora nchini humo. Alizaliwa Tabora, Tanzania mwaka 1987, alianza kucheza soka la kulipwa akizichezea Moro United, African Lyon, Simba SC, na Mbeya City.

10. Athuman Idd

Athuman Idd

Athuman Idd kwa sehemu kubwa anajulikana kama moja ya wachezaji wakubwa zaidi wa Kitanzania wa mpira wa miguu. Alizaliwa nchini Tanzania mwaka 1988 na alianza kucheza soka katika klabu ya Simba SC. Baada ya kuonesha kiwango cha kuvutia Simba, alijiunga na Yanga SC na kuwa sehemu muhimu ya timu hiyo.

Hitimisho

Mandhari ya mpira wa miguu wa Kitanzania umekuwa ukibarikiwa na baadhi ya wachezaji wenye vipaji zaidi miongo ya karibuni, ikihusisha Athuman Idd, Mbwana Samatta, Khamis Mcua, na Hadji Mberwa. Wachezaji hawa wakubwa wamechagiza mafanikio makubwa kwenye mchezo huu nyumbani na kimataifa. Mafanikio yao ni hamasa kwa vizazi vya sasa na vijavyo vya wachezaji mpira wa miguu wa Kitanzania ambao watapambana kuwa wakubwa kama tu malejendari hawa walivyofanya kabla yao.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je! Ni Mchezaji Yupi Mwenye Thamani Zaidi Nchini Tanzania?

Mchezaji Mwenye Thamani Zaidi Nchini Tanzania kwa mapana anachukuliwa kuwa Ally Samatta mwenye thamani ya sokoni ya Euro milioni 3.1.

Je! Nani Ndiye Mchezaji Maarufu wa Mpira wa Miguu Barani Afrika?

Mchezaji mpira wa miguu maarufu zaidi barani Afrika bila shaka ni Mohamed Salah, mshambuliaji huyu wa kimataifa wa Misri kwa sasa anaichezea Liverpool FC katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Je! Nani Ndiye Mchezaji Namba 1 wa Mpira wa Miguu kwa Sasa?

Mchezaji namba moja wa mpira wa miguu kwa sehemu kubwa anachukuliwa kuwa Sadio Mane.

Soma Zaidi

Je, unahitaji kuwa wa kwanza kupata taarifa mbalimbali?

Subscription was successfully completed.