Wanacheza – Unashinda Jiunge sasa
Mwanzo / / Wachezaji 10 Matajiri Zaidi wa Mpira wa Miguu: Chati Isiyotabirika ya Wataalamu

Mpira wa miguu ni moja ya michezo maarufu na inayolipa zaidi ulimwenguni, na baadhi ya mastaa wake wakubwa wamejilimbikizia viwango vikubwa vya utajiri. Huku wachezaji mpira wa miguu wakiingiza mamilioni kila mwaka kutoka kwenye mishahara yao, bonasi, matangazo, na biashara nyingine, haishangazi kwamba ni miongoni mwa wanamichezo matajiri zaidi.

Katika makala hii, tunawaangazia wachezaji kumi matajiri zaidi wa mpira wa miguu. Wachezaji hawa wameingiza pesa nyingi kupitia kucheza mpira na uwekezaji nje ya uwanja. Kutoka kwa Cristiano Ronaldo hadi Lionel Messi hadi kwa Neymar Jr., hawa ni baadhi ya wachezaji wanaolipwa vizuri zaidi katika historia yote ya michezo ambao wametengeneza bahati kubwa sana kutokana na vipaji vyao vya kuvutia.

1. Faiq Bolkiah

  • Utajiri: Dola za Marekani Bilioni 20

Faiq Bolkiah – mchezaji mwenye utajiri wa dola za Marekani bilioni 20

Faiq Bolkiah ni moja ya wachezaji matajiri zaidi ulimwenguni na mmoja wa wanafamilia ya kifalme ya Brunei, kitu kinachomfanya kuwa mchezaji mpira tajiri zaidi ulimwenguni. Utajiri wake mkubwa unatokana na uwekezaji wa familia yake na kucheza kwake mpira katika vilabu vikubwa kama vile Marítimo B na Chonburi.

2. Lionel Messi

  • Utajiri: Dola za Marekani Milioni 600

Lionel Messi – Supastaa wa viwango vya juu kwenye mpira wa miguu

Lionel Messi anachukuliwa kuwa moja ya wachezaji mpira wa miguu wakubwa zaidi wa wakati wote, na pesa yake itokanayo na kucheza mpira inaakisi hilo. Mikataba yake na Barcelona, Nike, na matangazo mengine yamemuingizia mamilioni. Pia ana mkataba wa maisha na manguli wa vifaa vya michezo Adidas, kitu kinachompa kipato cha nyongeza.

Messi anachukuliwa kuwa moja ya wanamichezo wanaolipwa zaidi ulimwenguni na anakadiriwa kuingiza karibia dola za marekani milioni 80 kwa mwaka, kitu kinachomfanya kuwa moja ya wachezaji wa mpira wa miguu matajiri zaidi ulimwenguni.

Lionel Messi anamiliki mali huko Miami, Barcelona, Ibiza, na nyumbani kwao Rosario, Argentina. Lionel Messi anamiliki magari kadhaa, ikihusisha Ferrari 335 S Spider Scaglietti, Pagani Zonda Tricolore, Audi RS6, Audi A7, Audi Q7, Mercedes SLS AMG, Maserati Gran Turismo MC Stradale, Ferrari F430 Spyder, Range Rover Sport, Range Rover Vogue, and Cadillac Escalade. Anamiliki boti ya kifahari kitu kinachomfanya kuwa mchezaji wa mpira wa miguu namba 2 kwa utajiri zaidi ulimwenguni.

3. Cristiano Ronaldo

  • Utajiri: Dola za Marekani milioni 490

Cristiano Ronaldo – Mcheza mpira wa miguu anayelipwa zaidi

Cristiano Ronaldo ni mchezaji mpira wa miguu anayelipwa zaidi na moja ya wachezaji matajiri zaidi wa mpira wa miguu ulimwenguni. Supastaa huyu wa Kireno ameingiza mamia ya mamilioni katika kipindi chote cha uchezaji wake kwenye baadhi ya vilabu vikubwa, ikihusisha Manchester United, Real Madrid, na Juventus. Pia ana rundo la mikataba ya matangazo na makampuni makubwa kama vile Nike, Livescore, Tag Heuer, Herbalife, Armani, Sacoor Brothers suits, na Monster headphones.

Cristiano Ronaldo anamiliki mali huko Lisbon, Madeira, Turin, Madrid, na Manchester. Pia anamiliki boti ya kifahari yenye urefu wa futi 88 iliyo na thamani ya Euro milioni 5.5 na ndege binafsi. Cristiano Ronaldo ana magari mengi, yanayohusisha Rolls-Royce Cullinan, Ferrari F12 TDF, Lamborghini Aventador, Bugatti Centodieci, Maserati GranCabrio, Porsche 911 turbo S, Ferrari F430, Mercedes Benz Brabus G65, Bugatti Chiron, Audi RS7, Mercedes Benz GLE63s AMG, Rolls-Royce Phantom Drophead, Ferrari 599 GTO, Bentley Continental, Mercedes Benz S65, Veyron Grand Sport Vitesse, Chevrolet Camaro ZL1 na Ferrari Monza SP1.

4. David Beckham

  • Utajiri: Dola za Marekani milioni 450

David Beckham – Nyota Mwingereza wa mpira wa miguu

David Beckham ni mchezaji mashuhuri wa mpira wa miguu ambaye ameingiza mamilioni kwa kucheza mpira. Alitengeneza mamilioni kwa kuvichezea baadhi ya vilabu vikubwa, kama vile Manchester United na Real Madrid. Kwa kuongezea mshahara wake, pia aliingiza pesa kupitia matangazo na makampuni kama Adidas, Konami, Tudor, Kent & Curwen, Diageo, Jaguar, n.k. Beckham anakadiriwa kuingiza karibia dola za Marekani milioni 50 kwa mwaka. David Beckham alitengeneza zaidi ya dola za Marekani milioni 280 kupitia matangazo na makampuni na dola za Marekani milioni 250 kutokana na mshahara kwenye mpira wa miguu, akiingiza kitita cha dola za Marekani milioni 450 kwa ujumla.

David Beckham anamiliki mali kadhaa London, Miami, na Dubai. Pia anamiliki boti ya kifahari. Anamiliki magari mengi sana kama McLaren MP4-12C Spider, Rolls Royce Phantom, Aston Martin V8 Vantage X-Pack Volante, Aston Martin V8 Vantage, X-Pack Volante, Cadillac Escalade ESV, Ferrari 360 Spider, Ferrari 612 Scaglietti, Lamborghini Gallardo, 1998 Ferrari 550 Maranello and Bentley Bentayga.

5. Dave Whelan

  • Utajiri: Dola za Marekani milioni 220

Dave Whelan – Milionea wa EPL

Dave Whelan ni moja ya wachezaji matajiri zaidi wa mpira wa miguu ulimwenguni na alitengeneza uwekezaji wenye faida sana wakati akicheza soka la kulipwa. Aliingiza mamilioni akivichezea vilabu kama Blackburn Rovers na Crewe Alexandra. Utajiri wake pia unatokana na yeye kumiliki timu ya Ligi Kuu ya Uingereza Wigan Athletic na biashara kadhaa. Whelan anakadiriwa kuingiza karibia dola za Marekani milioni 30 kwa mwaka.

6. Neymar Jr.

  • Utajiri: Dola za Marekani milioni 200

Neymar Jr. – Shujaa wa Kibrazili kutoka PSG

Neymar ni moja ya wachezaji mpira wa miguu wenye kipaji zaidi ulimwenguni, na pesa anayoingiza inaakisi hilo. Ametengeneza mamilioni akivichezea baadhi ya vilabu vikubwa, kama vile Barcelona na Paris Saint-Germain. Kwa kuongezea kwenye mshahara wake, anaingiza pia pesa nyingi kutoka kwenye matangazo na makampuni kama vile Epic Games,  Puma, Flutter Entertainment, Qatar Airways, Triller, and Red Bull, miongoni mwa mengine. Neymar anakadiriwa kuingiza karibia dola za Marekani milioni 75 kwa mwaka.

Neymar ana modeli kadhaa za kifahari miongoni mwa magari yake. Anamiliki Lamborghini Veneno, Ferrari 458 Italia, Audi R8 Spyder V10 Plus, Lykan Hypersport, Maserati Mc12, Porsche Panamera Turbo, Mercedes AMG GT S, Range Rover SVA, and Mercedes-Benz G63 AMG.

7. Zlatan Ibrahimovic

  • Utajiri: Dola za Marekani milioni 190

Zlatan Ibrahimovic – mchezaji nguli wa mpira wa miguu

Zlatan Ibrahimovic ni moja ya wachezaji mashuhuri ulimwenguni na amejilimbikizia utajiri wa kuvutia wakati akicheza soka la kulipwa. Aliingiza mamilioni akivichezea baadhi ya vilabu vikubwa, kama vile Barcelona, Juventus, na Paris Saint-Germain. Kwa kuongezea mshahara wake, pia ana mkataba wa matangazo na Volvo.

Zlatana anamiliki kampuni ya vifaa vya michezo, A-Z Sportswear, ambayo aliianzisha 2016. Pia alianzisha Ibrahimovic Parfums akishirikiana na Olivier Pescheux. Zlatan ana magari kadhaa katika karakana yake na ndege ya kifahari. Magari katika karakana ya Ibrahimovic ni pamoja na Porsche 918 Spyder, Maserati Gran Turismo MC, Ferrari LaFerrari, Ferrari Monza SP2, Ferrari Enzo, and Volvo XC70.

8. Wayne Rooney

  • Utajiri: Dola za Marekani milioni 160

Wayne Rooney – Mchezaji shujaa wa mpira wa miguu Mwingereza

Wayne Rooney ni mchezaji mpira wa miguu mashuhuri Mwingereza ambaye ameingiza mamilioni kipindi anacheza soka la kulipwa. Aliingiza mamilioni akivichezea vilabu vya Manchester United, Everton, na D.C. United. Kwa kuongezea mshahara wake kama kocha, pia anaingiza pesa kupitia matangazo na makampuni kama vile Asda, Nike, Ford, Coca-Cola, and Nokia.

Rooney anapenda sana mali zisizohamishika. Ana nyumba huko Cheshire, Uingereza; nyumba ya kupangisha huko Port Charlotte, Florida; na jumba la kifahari huko Barbados villa. Rooney anamiliki magari kadhaa. Magari hayo yanahusisha Bentley Continental GT, Range Rover Evoque (Overfinch), BMW i8, Audi Q7, Lamborghini Gallardo, Aston Martin Vanquish S, Audi RS6 Avant, Mercedes CLS Coupe, Range Rover Vogue (Overfinch), BMW X5.

9. Gareth Bale

  • Utajiri: Dola za Marekani milioni 125

Gareth Bale – mwakilishi wa mtindo wa maisha ya lakshari

Gareth Bale ni moja ya wachezaji mpira wa miguu anayesifiwa sana ulimwenguni, akiwa amevichezea baadhi ya vilabu vikubwa, kama vile Tottenham Hotspur, Real Madrid, na Los Angeles FC. Utajiri wake unatokana na mshahara wake na matangazo na makampuni kama vile Adidas, Konami, Foot Locker, na Nissan Motor. Bale ni mwanzilishi wa Primesure Limited.

Gareth Bale anamiliki Audi R8 Spyder, Audi Q7, Lamborghini Aventador Roadster, Mercedes Class C63 AMG Coupe, na Range Rover. Pia anamiliki jumba la kifahari huko Cardiff, Uingereza, na eneo la La Finca lililopo Madrid, Hispania.

10. Andrés Iniesta

  • Utajiri: Dola za Marekani milioni 120

Andrés Iniesta – Nyota wa mpira wa miguu Muhispania

Andrés Iniesta ni nyota wa mpira wa miguu Muhispania ambaye alitengeneza mamilioni akikichezea moja ya vilabu vikubwa zaidi ulimwenguni, Barcelona, kabla hajahamia Vissel Kobe nchini Japani. Iniesta anamiliki biashara ya mvinyo na anaingiza pesa kupitia matangazo na Nike na EA sport. Iniesta anakadiriwa kuingiza karibia dola za Marekani milioni 30 kwa mwaka kwenye klabu yake ya sasa. Iniesta anamiliki Nissan, Bugatti Veyron, Audi, and Range Rover, miongoni mwa magari mengine.

Hitimisho

Hivyo, hii hapa ndio chati yetu ya ujumla ya wachezaji 10 matajiri zaidi ulimwenguni. Mpira wa miguu ni moja ya michezo maarufu na inayolipa zaidi ulimwenguni. Baadhi ya mastaa wake wakubwa wamejilimbikizia viwango vikubwa vya utajiri.

Huku wachezaji wa mpira wa miguu wakiingiza mamilioni kila mwaka kutoka kwenye mishahara yao, bonasi, matangazo, na biashara nyingine, haishangazi kwamba ni miongoni mwa wanamichezo wenye utajiri zaidi. Tu follow Parimatch kwa taarifa za ndani zaidi na dondoo za kubeti!

Soma Zaidi

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je! Kina Nani Ndiyo Wachezaji 10 Matajiri Zaidi wa Mpira wa Miguu?

Wachezaji 10 matajiri zaidi wa mpira wa miguu ulimwenguni ni Faiq Bolkiah, Lionel Messi,  Cristiano Ronaldo, David Beckham, Dave Whelan, Neymar Jr., Zlatan Ibrahimovic, Wayne Rooney, Gareth Bale, na Andrés Iniesta.

Je! Nani Ndiye Mchezaji Namba 1 Tajiri Zaidi Ulimwenguni?

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji anayelipwa zaidi ulimwenguni baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu wenye thamani ya €200m (£177m) kwa mwaka na klabu ya huko Saudi, Al-Nassr.

Je! Nani Ndiye Mchezaji Mpira wa Miguu Tajiri Zaidi Afrika 2022?

Wadhifa wa mchezaji mpira wa miguu tajiri zaidi barani Afrika kwa mwaka 2022 bado haupo wazi, kutokana na kwamba hali ya kifedha katika anga la soka la Afrika hubadilika kila wakati.

Je! Nani Ndiye Mchezaji wa Kiafrika Anayelipwa Zaidi?

Mohammed Salah kwa sasa ndiye mchezaji wa Kiafrika anayelipwa zaidi. Winga huyu Mmisri kwa sasa anaichezea Liverpool FC na anaingiza Euro milioni 16.8 kwa mwaka. Salah ni mashuhuri nchini mwake na ulimwenguni kote.

Je, unahitaji kuwa wa kwanza kupata taarifa mbalimbali?

Subscription was successfully completed.