Wanacheza – Unashinda Jiunge sasa
Mwanzo / / Wachezaji 10 Bora wa Kabumbu wa Uingereza wa Muda Wote Waliowahi Kucheza Kandanda

Kama mojawapo ya vinara wa mpira wa miguu duniani, mara kwa mara Uingereza hutoa baadhi ya wachezaji bora zaidi. Kwenye hii makala hapa chini, kampuni ya kubashiri Parimatch imeorodhesha wachezaji 10 wenye vipaji maarufu na mashuhuri kutoka Kiingereza, na maelezo ya kwanini kila moja ya hawa wanasoka anafaa kushika namba aliyoishika kwenye orodha hii.

Wachezaji 10 Bora wa Muda Wote wa Soka Kutoka Uingereza

Uingereza ina Kombe la Dunia moja pekee, lakini uwezo wao wa kuzalisha wanasoka wa daraja la juu bado haujatiliwa mashaka. Kutoka kwenye mamia – kama sio maelfu – ya wanasoka wa ajabu, tumewachagua wachezaji 10 bora zaidi. Endelea kusoma ili ugundue ni nani aliyetengeneza orodha ya wachezaji wanaokuwezesha wewe kubashiri ukiwa na mwanzilishi wa michezo wa Parimatch. Orodha ya wachezaji bora wa soka kutoka nchini Uingereza.

Cheo

Mchezaji mpira Mataji ya EPL Kombe la Dunia waliloshinda

Magoli

1 Sir Bobby Charlton 3 1 260
2 Bobby Moore 0 1 28
3 Gordon Banks 0 1 0
4 Jimmy Greaves 1 1 469
5 Wayne Rooney 5 0 313
6 Steven Gerrard 0 0 190
7 Paul Scholes 11 0 155
8 Alan Shearer 1 0 379
9 David Beckham 10 0 129
10 Frank Lampard 3 0 274

Wachezaji 10 bora wa Soka kutoka nchini Uingereza

Namba 10 – Frank Lampard

Frank Lampard – A Talented Midfielder

Kwa kawaida viungo washambuliaji wanatakiwa kutengeneza viungo bora, kutengeneza nafasi na kutoa pasi za magoli kwa wachezaji wengine. Hii ilikuwa ni kabla ya Frank Lampard kufafanua tena jukumu lake hilo. Uchezaji wake wa kumuwezesha kufunga mabao 274 katika maisha yake ya kabumbu unatosha kwa mshambuliaji yeyote wa kiwango cha juu, lakini alifunga magoli hayo mengi akiwa kwenye safu ya kiungo.

Kama baba yake, Lampard alianza uchezaji wake akiwa na West Ham, lakini ilikuwa ni Chelsea ambapo alikua ni kiungo mwenye kiwango cha kimataifa, akishinda mataji matatu ya ligi na vilevile taji la UEFA Champions League.

Takwimu moja ya kushangaza kutoka kwenye kazi ya Lampard ni kuwa alimaliza kwa takwimu mbili kwenye safu ya magoli kwa misimu 10 mfululizo. Jambo lingine la kushangaza ni kuwa alifunga magoli manne mara mbili kwenye mchezo mmoja – kwanza dhidi ya Derby County na kisha dhidi ya Aston Villa, klabu ambayo ina Mtanzania, Mbwana Samatta aliyecheza kwa takriban muongo mmoja baadaye.

Lampard anaingia kwenye orodha hiyo kwa kuondoa majina kama vile Paul Gascoigne na Harry Kane, ambapo ukosefu wao wa mafanikio kwenye timu ulihesabiwa kwao.

Namba 9 – David Beckham

David Beckham - England Football Superstar

Mfumo, mitindo, maisha tajiri na sura nzuri ya David Beckham vinaweza kuwadanganya watu wengine wakadharau uwezo wake wa kucheza soka na mafanikio yake, lakini jambo la msingi ni kuwa ni mpiga krosi bora zaidi wa kwenye mchezo ambaye umewahi kumuona.

Becks, kama alivyokuwa akijulikana kwa upendo, alikuwa ni mpiga krosi na mtaalamu wa kudondosha mipira kwenye vichwa vya washambuliaji kwa usahihi wa uhakika. Lakini alama yake ya kibiashara ilikuwa ni umahiri wake kwenye kupiga mipira ya adhabu, ambao aliutumia sana wakati wa kazi yake ya kusisimua awapo dimbani.

Alishinda mataji sita ya ligi akiwa na klabu ya soka ya Manchester United kabla ya kutoelewana na Sir Alex Ferguson kumfanya kuchagua ahamie Real Madrid, ambapo alishinda taji lingine la ligi. Baadaye, alishinda vikombe viwili vya MLS nchini Marekani kisha akarejea Ulaya na kunyanyua taji la Ligue 1 akiwa na PSG na kuhitimisha maisha yake ya soka barani Ulaya na kwingineko.

Namba 8 – Alan Shearer

Alan Shearer – A Prolific England Striker

Ingawa rekodi yake inapaswa kuvunjwa siku moja hivi karibuni na mshambuliaji wa asili hiyo (Harry Kane), Alan Shearer anabakia kuwa ndiye mfungaji bora zaidi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kwa sasa, akiwa na magoli 260 kwenye jina lake.

Mshambulizi mahiri, Shearer alikuwa wa kipekee kwa njia zake yeye mwenyewe kwani alichagua kutocheza kwa wapinzani wa jadi nchini Uingereza. Sir Alex Ferguson huyo ni mmoja wa makocha bora wa soka wa wakati wote alimfukuzia Manchester United bila kikomo, lakini Shearer hakutetereka.

Uamuzi wake wa kuchezea timu kama vile Blackburn Rovers na Newcastle United ulimaanisha kuwa alishinda taji moja tu la ligi (na Blackburn), lakini kimo chake kwenye soka la Uingereza kimekuwa ni cha juu sana kwenye matokeo.

Namba 7 – Paul Scholes

Paul Scholes - An Iconic Midfielder from England

“Yeye ndiye mtu bora zaidi kwenye nafasi ya kiungo wa kati nimemuona kwenye miaka 15, 20 iliyopita,” – Xavi.

Hivi ndivyo nguli wa zamani wa Hispania na Barcelona, Xavi alisema kuhusu Paul Scholes, na wakati mtu anayetoa pasi za aina hiyo ana maoni kama hayo juu ya mtu, hakika ni lazima iwe kweli.

Vikosi vya Sir Alex vya Manchester United vya miaka ya 1990 na 2000 vilikuwa na wanasoka wengi wenye kasi na wafungaji magoli kama vile Eric Cantona, David Beckham, Ruud Van Nistelrooy, na wengineo, lakini mapigo ya moyo ya timu hizo zote yalikuwa ni kwa mhusika fulani aliyeitwa Paul Scholes.

Hakukuwa na pasi ya soka ambayo Scholes hakuweza kuitendea vyema kwa kupepesa macho. Alidhibiti mchezo na kuamuru kasi yake kama vile Andrea Pirlo, Xabi Alonso, na Xavi mwenyewe walivyofanya hapo baadaye.

Alishinda mataji 11 ya ligi – zaidi ya mtu mwingine yeyote kwenye orodha na alimaliza akiwa na magoli ya heshima 155 kutoka katikati mwa uwanja.

Namba 6 – Steven Gerrard

Steven Gerrard - A Successful Leader

Steven Gerrard alicheza soka maisha yake yote kwenye Ligi Kuu ya Uingereza lakini hakushinda hata mara moja. Licha ya hayo, anaweka orodha hiyo, ambayo inaonesha ni aina gani ya uwezo ambao ni lazima alikuwa nao.

Gerrard alikuwa na kila kitu ambacho kiungo wa kati alikihitaji kuwa nacho. Alikuwa na pasi ndani yake, alikuwa na mapambano makubwa ndani yake, alikuwa na magoli ndani yake, na zaidi ya yote, alikuwa na uongozi ndani yake. Kwa kweli, hakukuwa na kitu ambacho asingeweza kukifanya.

Wakati taji la ligi lilipomkwepa licha ya kulikaribia, wakati bora zaidi wa Gerrard ulikuja Ulaya wakati alipotaka kutwaa ubingwa akiwa na Liverpool. Kwanza, kulikuwa na goli la muda mrefu dhidi ya Olympiacos ili kuwaweka Wekundu hao kwenye kinyang’anyiro hicho. Kisha yakaja mafanikio yake ya taji alipochochea pambano la Liverpool kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa, na kuikokota timu yake kutoka 3-0 hadi mapumziko na kupata ushindi maarufu dhidi ya timu iliyojaa nyota ya AC Milan.

Namba 5 – Wayne Rooney

Wayne Rooney – True English Football Wunderkind

Uingereza haijawahi kuwa na mtu mwenye kipaji kama Wayne Rooney wakati wa ujana wake. Akiwa amebarikiwa na mwili mkubwa akiwa na umri mdogo, Rooney aliwika sana kwenye soka na hakutazama nyuma.

Alionesha kuwasili kwake kwenye hatua kubwa zaidi kwa goli la ushindi la dakika za lala salama kwa Everton dhidi ya Arsenal akiwa na umri wa miaka 16 kabla ya kuhamia Manchester United, ambapo alicheza kwa muda mwingi maishani mwake.

Mchanganyiko mkubwa wa kasi, nguvu, na ari, Rooney hakuzuilika akiwa dimbani na mmoja wa washambuliaji safi kabisa wa soka. Pia, alikuwa na kipaji cha kufunga magoli yenye umahiri. Aliunawa mpira walipocheza dhidi ya Newcastle na goli la kichwa kwenye mechi ya dabi ya Manchester utaishi katika kumbukumbu zetu kwa muda mrefu.

Namba 4 – Jimmy Greaves

Jimmy Greaves - Top Goalscorer of All Times

Si wengi wanaolikumbuka jina lake, mafanikio na uwezo wake, lakini wanaofahamu wanafahamu kuwa Jimmy Greaves alikuwa mfungaji bora na mwenye uwezo mkubwa zaidi kuwahi kucheza kabumbu la Uingereza. Greaves alianza kucheza kabumbu lake akiwa na Chelsea na kupachika magoli 132 katika mechi 169 pekee kwenye kampeni zake nne za kwanza za ligi kuu. Hilo lilimfanya avutiwe na wababe wa Italia, AC Milan, ambapo Greaves aliwachezea lakini bado alifunga magoli tisa katika mechi 13.

Kurejea Uingereza na Tottenham kulimfanya kufunga magoli mengine 268 katika mechi 381 pekee kabla ya kumaliza na timu kadhaa ndogo.

Wakati Shearer anashikilia rekodi ya ufungaji wa muda wote katika enzi ya Premier League, hata yeye hafiki popote pale ambapo Greaves alifikia 357 katika ligi kuu ya Uingereza.

Namba 3 – Gordon Banks

Gordon Banks – The Greatest Goalkeeper

Kwa urahisi, kipa bora zaidi wa Uingereza wa wakati wote, Gordon Banks hakuona mafanikio mengi ya timu katika kazi yake ya klabuni. Alishinda tu vikombe viwili vya Ligi – la kwanza akiwa na Leicester City na lingine akiwa na Stoke City. Mashabiki wa kandanda ndani ya Tanzania tungeikumbuka Leicester City kwani hiyo ndiyo klabu ambayo Adi Yussuf wetu alianzia maisha yake ya soka.

Lakini bila kusitasita, turudi kwenye mada. Banks, licha ya kukosa mafanikio ya klabu, aliteuliwa kuwa Golikipa Bora wa Mwaka wa FIFA kwa miaka sita mfululizo – hiyo ndiyo ilikuwa kwenye mafanikio yake kipindi cha nyuma.

Lakini kile ambacho hakufanikiwa akiwa na Leicester na Stoke, alikifanya akiwa na timu ya taifa ya Uingereza. Alikuwa kipa mkuu wa Uingereza katika kampeni yao pekee ya kushinda Kombe la Dunia mwaka 1966. Miaka minne baadaye, katika mchezo muhimu dhidi ya Brazil, aliokoa mpira kwa njia nzuri sana hata akamshangaza Pele. Bila ya ugonjwa wake, huenda Uingereza isingepoteza kwa Ujerumani Magharibi kwenye hatua ya robo fainali.

Namba 2 – Bobby Moore

Bobby Moore - A Top England Defender

Bobby Moore alikuwa ni mlinzi kwa muongo kabla ya wakati wake. Alikuwa ni mshindi bora wa mpira lakini alikuwa na raha sawa na mpira. Mfikirie kuwa yupo kati ya John Terry anayecheza mpira mkali na Rio Ferdinand. Uwepo wake pekee ulidhihirisha imani kwa wachezaji wenzake.

Mpaka sasa, anabakia kuwa ndiye nahodha pekee wa Uingereza kuiongoza Three Lions kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia. Ilikuwa ni uchezaji wake mzuri wa safu ya ulinzi ya Waingereza ambao uliifanya safu ya ulinzi yao kuwa bila ya makosa hadi nusu fainali ilipovunjwa kwa mara ya kwanza.

Mnamo mwaka 1970 vilevile, licha ya matatizo yake ya nje ya uwanja (soma Bogota Bracelet), aliweza kuweka utulivu na alikuwa kinara wa timu ya Uingereza ambayo iliwazuia mabingwa wa baadaye wa Brazil kwa goli moja tu. Mchezo wake dhidi ya Jairzinho maarufu bado haujakumbukwa kwenye soka linalopendwa na mashabiki.

Hata hivyo, alicheza sehemu kubwa ya maisha yake ya klabu akiwa na West Ham na hakuwa na sifa nyingi za kuzionesha kwenye timu juu ya hilo. Kombe la FA na Kombe la Washindi wa Kombe la Ulaya ni vyote alivyoshinda akiwa na Wagonga Nyundo, ambapo alikuwa ni nahodha kwa zaidi ya muongo mmoja.

Namba 1 – Bobby Charlton

Sir Bobby Charlton - A Living English Legend

Baadhi ya wachangiaji wakuu kwenye kampeni ya ushindi ya Uingereza ya Kombe la Dunia la mwaka 1966 walikuwa wamepunguza maisha ya klabu lakini si kwa Sir Bobby Charlton.

Baada ya kunusurika kwenye ajali mbaya ya ndege, kazi ya Charlton bila shaka ilifikia umbali ambao hakuna mchezaji wa Kiingereza aliyewahi kuukaribia. Alishinda mataji matatu ya ligi akiwa na klabu ya soka ya Manchester United pamoja na Kombe la FA kwenda na Kombe la Ulaya katika msimu wa miaka ya 1967-68.

Pia, alitajwa kuwa ni mshindi wa Ballon d’Or mwaka 1966 na alimaliza akiwa mshindi wa pili katika gemu nyingine mbili.

Ukiinua uso na kutazama kazi nzima ya Charlton, itakuwa wazi unaona kuwa hakukuwa na chochote ambacho hakuweza kukifikia, ndiyo maana anakubalika kwa pamoja kama Muingereza mwanasoka mkubwa kuwahi kutokea kwa wakati wote.

Lakini tukifafanua tu kazi yake katika suala la vikombe na vikombe itakuwa ni dhuluma kwenye uwezo wake safi wa kucheza soka dimbani. Sir Bobby, kama alivyojulikana pia, alikuwa ni kiungo mahiri na mwenye uwezo wa ajabu wa kupiga mashuti, stamina na uongozi. Pia, alikuwa fiti sana, ambayo ilimuwezesha kuendelea kucheza hadi akiwa mzee sana wa umri wa miaka 43.

Muhtasari

Karibia kila wakati kunakuwa na orodha ya 10 bora, na uteuzi wa mtaalam mmoja unaweza kutofautiana na wa mtu mwingine. Hata hivyo, orodha ya juu ya wachezaji bora wa soka iliyoandaliwa na wataalam wetu kwenye Parimatch inatoa uzito maalum kwenye mafanikio ya timu ya wachezaji, sifa binafsi pamoja na athari kwenye mchezo.

Hakuna mchezaji hata mmoja kwenye orodha ambaye yupo kwenye timu kwa sasa, lakini baadhi ya wachezaji wanaocheza, kama vile Harry Kane na Phil Foden, wanaweza wakati fulani kulazimisha kuingia kwenye 10 bora.

Ili kuamua kama mchezaji yeyote wa kandanda wa Uingereza anaweza kuingia kwenye orodha, mashabiki wa soka ndani ya Tanzania wanapaswa kutazama Ligi Kuu ya Uingereza. Wakati wa kutazama, wanaweza pia kutumia maarifa yao ya mchezo wa kubashiri mtandaoni leo na Parimatch kupitia tovuti yetu au app.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je, ni wachezaji gani bora wa soka Uingereza?

Sir Bobby Charlton, Bobby Moore, na Gordon Banks ni miongoni mwa wachezaji bora wa soka wa Uingereza.

Nani ni mwanasoka maarufu zaidi nchini Uingereza?

David Beckham ndiye mwanasoka maarufu zaidi nchini Uingereza kutokana na mafanikio yake kwenye kandanda na kazi yake ya mitindo.

Nani ni mchezaji wa soka anayependwa zaidi nchini Uingereza?

Sir Bobby Charlton ndiye mchezaji wa soka anayependwa zaidi nchini Uingereza kwa sababu ya kazi yake isiyo na doa.

Nani ni mchezaji mwenye utajiri zaidi wa mpira wa miguu Uingereza?

David Beckham ndiye mchezaji tajiri zaidi wa mpira wa miguu wa Uingereza, na ana wastani wa utajiri wa dola milioni 450.

Je, unahitaji kuwa wa kwanza kupata taarifa mbalimbali?

Subscription was successfully completed.