Wanacheza – Unashinda Jiunge sasa
Mwanzo / / Kiasi Wanacholipwa Wanasoka

Soka, ambalo mara nyingi huwa ni kazi ya kitaaluma na mchezo mzuri, imeteka mioyo ya mamilioni ya mashabiki wa nchini Tanzania. Msisimko, raha yake, na shauku ya kuitazama timu yako pendwa ikicheza mpira uwanjani hakika ni kitu kizuri sana. Ila, je, umeshawahi kujiuliza ni pesa kiasi gani ambazo wachezaji wako uwapendao wa soka wanalipwa kwa kucheza gemu wanazozipenda sana? Hapa, Parimatch, tunachunguza mishahara inayovutia macho ya wachezaji wa soka, kuanzia Ligi ya Kitaifa ya Kabumbu mpaka Ligi Kuu na Kombe la Dunia.

Ni imani ya Parimatch kuwa kuuelewa wastani wa mapato kwa wachezaji wa kabumbu kunaweza kukusaidia sana kwenye kufanya maamuzi sahihi juu ya nani wa kumbetia. Pia, tutafahamu wastani wa mishahara kwenye taaluma nyingine za kandanda.

Je, Wanasoka wa Kulipwa Hutengeneza Kiasi Gani cha Pesa?

Hakika, kuna watu ambao wanaweza kujiuliza ni kiasi gani cha pesa ambacho wachezaji wa soka wanalipwa na pia ni kiasi gani ambacho wachezaji wa kabumbu wanakipata kwa mwaka na wachezaji wa kabumbu wanalipwaje kwa kila gemu. Baadhi ya watu hufikiri kuwa wachezaji wa Ligi Kuu pekee ndio wanaolipwa sana, kwa hiyo kwenye hizi sehemu zinazofuatia, tutaona ni kiasi gani cha pesa wanazolipwa wachezaji wa ndani kwenye soka, ni kiasi gani cha pesa ambacho wachezaji mahiri wa kabumbu wanakitengeneza, na wastani wa malipo kwenye michezo ya Ligi Kuu ya Kitaifa (NFL) pamoja na kabumbu kwa ujumla na mshahara wa wachezaji hao.

Fahamu Kiasi cha Pesa Wanacholipwa Wachezaji wa Kabumbu wa Kawaida

Kandanda ina baadhi ya wachezaji wake wanaoishi ndoto zao. Ila, ni kiasi gani cha mkwanja ambao wachezaji wanaweza kukitengeneza kwa mwaka? Kwa wastani, huweka mfukoni takriban $32,476 kwa mwaka. Ila, kumbuka kwamba hiyo haiishii hapo tu. Kiasi wanachovuna hutegemea wapi wanacheza, umri, afya, uchezaji, uzoefu na namna wasakata kabumbu hawa walivyo bora.

Tuzo kubwa ipo kwenye Ligi ya Kitaifa ya Kandanda – moja ya michuano mikuu ya soka huko Marekani. Kuna takriban fursa 1,500, ila ukibahatika kuingia, unaweza kuwa unakunja mpunga mzuri sana, na kutengeneza mamilioni kila mwaka!

Fahamu Mkwanja wa Wanasoka kwa Mwaka na kwa Kila Gemu

Baada ya kila mwaka wa kwanza wa mchezaji kwenye Ligi ya NFL, mshahara wake wa chini unapaa hadi $28,125 kwa kila gemu ya kawaida kwa kila msimu, jumla ya $450,000 kwa mwaka. Baada ya miaka miwili, mchezaji wa NFL hulipwa mshahara wa msingi wa $32,812 kwa kila gemu, sawa na $525,000 kwa kila mwaka. Kila mchezaji wa NFL aliye chini ya mkataba hulipwa kila wiki kuanzia mwanzo wa msimu hadi mwishoni.

Uwanja wa mpira wa miguu

Wanasoka vya Akademi Wanalipwaje?

Endapo nawe unajiuliza, wacheza soka wa ndani hulipwa kiasi gani cha mshahara, basi hapa unapata majibu. Mshahara wa wastani kwa wachezaji wote wa NFL ni takriban $860,000, ambao ni mshahara wa chini kabisa, na wanaoshiriki kucheza mwaka wa kwanza wanapata kima cha chini cha $435,000. Wakati wachezaji wa nyuma upande wa juu huwa wanaweza kutengeneza zaidi ya $25 hadi $30 milioni kwa mwaka, wastani wa mshahara kwa sehemu za kati zote ni $5,766,000, na mapato ya wastani ya $1,100,000 ingawa mishahara ya mtu binafsi kwa wale wanasoka wa akademi hutofautiana kulingana na uzoefu na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.

Kama tulivyonena hapo mwanzo, kuna takriban nafasi 1,500 pekee kwenye ligi ya NFL, na kuifanya kuwa ni kazi yenye ushindani mkubwa sana. Maisha ya Ligi ya Soka ya Kitaifa kwa kawaida huwa ni kati ya miaka 2-10. Wakati huo wote, wanafurahia mapato makubwa sana na wanaweza kupata mapato ya ziada kupitia malipo ya baada ya msimu, motisha, bonasi za kuchaguliwa, bonasi za mazoezini, bonasi za kuorodheshwa, bonasi za kusaini mikataba, ridhaa za matumizi kwenye makampuni pamoja na kushiriki kwenye vyombo vya habari. Mapendekezo ya kutumika kuyatangaza makampuni ni aina ya utangazaji ambao hutumia picha na majina la mchezaji kufanya utambuzi na uaminifu kwenye bidhaa au huduma kadhaa.

Wachezaji Bora wa Soka Wanaolipwa Zaidi Mwaka 2023-2024

Mishahara ya wachezaji bora wa kulipwa inaendelea kupanda kwa kasi sana. Hii hapa ni orodha ya wachezaji 10 bora wa soka wanaolipwa zaidi kwa msimu wa mwaka 2023-2024 kuanzia wale wanaocheza kwenye Ligi Kuu na La Liga, Ligue 1, Kombe la Dunia, Manchester United hadi kule PSG. Wafuatao ni wanakabumbu wanaolipwa zaidi na wastani wa mshahara ambao kila mmoja anapokea.

1. NEYMAR JR (AL HILAL) – $240 MILIONI / MWAKA

Neymar, anayesifika kwa umahiri wake wa Kibrazili na uwezo wake wa kucheza chenga usio na kifani ambaye alishinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2015, amekuwa ndiye kivutio kikubwa miongoni mwa wachezaji wa kandanda. Kutua pale Al Hilal kunatuma ujumbe mzito sana duniani: wameazimia kuanzisha utawala wao rasmi. Bei ya Neymar ya dola milioni 100 haileti ujuzi wake tu; hulinda chapa yao, sifa zao, na kujitolea kutoa burudani isiyo na kifani.kwenye soka.

2. CRISTIANO RONALDO (AL NASSR) – $173 MILIONI / MWAKA

Huyu mchezaji wa zamani wa timu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Manchester United, ambaye pia ni mshindi wa Ligi ya Mabingwa, Cristiano Ronaldo kwa sasa anashikilia taji la mwanakandanda anayelipwa fedha nyingi zaidi pia. Zaidi ya hayo, Ronaldo, ambaye mara nyingi huonekana kama ni ishara ya kujitolea na aliye na juhudi zisizo na kiikomo, mara kwa mara huvunja rekodi kibao. Uhamisho wake kwenda klabu ya Al Nassr ulikuwa ni wakati wa kihistoria, ukisisitiza matarajio ya klabu hiyo. Akiwa na mapato ya jumla ya dola milioni 200, anajumuisha utajiri na mvuto wa ulimwengu wa kandanda.

Wachezaji mpira wa akademi

3. KARIM BENZEMA (AL-ITTIHAD) – $172 MILIONI / MWAKA

Benzema, mchezaji mashuhuri wa zamani wa Real Madrid ambayo inashiriki La Liga, analeta mchanganyiko wa utaalamu, vipaji, na uwezo wa kuvutia wa kufunga magoli pale Al Ittihad. Akiwa na bei ya dola milioni 200, ununuzi wake unaashiria zaidi ya kusajili tu mchezaji; inawakilisha uwekezaji unaotazamia makubwa hapo mbeleni na tamko la wazi la nia miongoni mwa watu wanaolipwa fedha nyingi.

4. KYLIAN MBAPPE (PSG) – $100 MILIONI / MWAKA

Yule mchezaji wa Ufaransa, Mbappe, anaendelea kuwa ndiye uso wa PSG na mmoja wa wanakabumbu wanaolipwa fedha nyingi zaidi. Chaguo lake la kubakia kwenye klabu hiyo ni ushahidi wa uaminifu wake na maono ya muda mrefu ya klabu ya soka ya PSG. Akiwa na malengo yake ya kustaajabisha na haiba ya kuvutia, mapato yake ya dola milioni 70 yanaashiria mchango wake mkubwa kwa timu ya PSG na soka la Ufaransa kwa ujumla.

5. N’GOLO KANTE (AL ITTIHAD) – $86 MILIONI / MWAKA

Stori ya Kante ni moja ya mambo yanayoburudisha sana na ni moja ya wanakabumbu ambao wanalipwa pesa ndefu zaidi. Kuibuka kwenye dunia ya soka sio jambo fupi la msukumo bali ni kujitoa mno. Al Ittihad, ikiitambua talanta yake na uwezo wake wa usakataji kandanda, ikafidia dola milioni 100, na kumfanya awe ni sehemu ya msingi ya mpango wao wa mafanikio. Alikuwa ni mmoja wa wachezaji bora wa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza miaka yake.

Wanasoka hawa watano, pamoja na mishahara yao ya kustaajabisha, wanaonesha mabadiliko ya mienendo ndani ya ulimwengu wa kandanda. Katikati ya masoko yanayoibukia na mikakati ya klabu inayoendelea kubadilika mara kwa mara, umuhimu wa vipaji vya wachezaji wa Kulipwa unaonekana zaidi kwa sasa kuliko hapo mwanzo. Vilabu vinapopanga mambo yao ya siku zijazo, wachezaji hawa wanajumuisha mchanganyiko wa athari ya kujituma na maono ya mbele. Mambo yao, ndani na nje ya uwanja, yamekuwa ni ushahidi wa ushawishi unaozidi kuongezeka sana kimataifa kwenye kandanda.

Ingawa takwimu zao zinaweza kuwa ni za ajabu, zinaonesha bidii, kujitolea, na talanta ya kipekee ya wanasoka hawa.

Wachezaji soka wa kulipwa

Je, Unamfahamu Mchezaji Anayelipwa Zaidi Hapa Tanzania?

Stephane Aziz Ki, ambaye ni kiungo wa miaka 26 kutoka nchini Burkina Faso, anashikilia sifa ya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye Ligi ya Tanzania. Kila mwezi anaweka kibindoni takriban $10,700, sawa na shilingi milioni 27 za hapa Tanzania, huku pia akipokea bonasi kubwa ya kusaini mkataba ambayo ni $215,000 alipowasili kwenye klabu ya soka ya Young Africans SC Juni mwaka 2022 akijiunga na wachezaji wengine wa soka kwenye Ligi Kuu ya NBC.

Ligi za Kulipwa na Namna Chaguzi za Kazi Zilivyo

Wachezaji hawaumii endapo hawatafika kwenye ligi ya NFL. Kuna hatua nyingine za kushangaza sana. Wachezaji wengine walipitia ligi ndogo kwanza ili kupata makali kabla ya maskauti wa NFL kuja kubisha hodi kwao. Ukikosea huko NFL bado zipo chaguzi nyingine kwa wachezaji wa kulipwa kando na NFL kama zinavyotajwa hapa chini:

  • Ligi ya Taifa ya Arena (National Arena League)XFL
  • Ligi ya Kandanda ya Ndani (Indoor Football League)
  • Gemu za Soka za Magharibi mwa Marekani (American West Football Conference)
  • Mabingwa wa Ligi ya Kandanda ya Ndani (Champions Indoor Football League)
  • Ligi ya Kandanda Inayoongozwa na Mashabiki (Fan-Controlled Football League)
  • Ligi ya Arena ya Marekani (American Arena League)

Pia, kuna ligi 3 za maendeleo ambazo zinakusudia kuwapa wachezaji nafasi ya kuboresha ujuzi wao kabla ya kuajiriwa kwenye NFL. Ligi ndogo kama hizi za kandanda ni:

  • Ligi ya Spring, ni fursa isiyo na malipo kwa wachezaji wa soka. (The Spring League)
  • Ligi ya Soka ya Maendeleo ya Gridiron, hapa wachezaji hulipwa mishahara. (Gridiron Developmental Football League)
  • Ligi ya Soka la Wapinzani, hapa pia wachezaji wanalipwa mishahara. (Rivals Professional Football League)

Uwanja wa mpira wa soka

Mahitaji ya Kuwa Mchezaji wa Soka wa Kulipwa

Mtu anaweza kujiuliza namna ya kuingia kwenye gemu za kulipwa. Yafuatayo ni baadhi ya mahitaji ya mtu anayetaka kuwa mwanasoka wa kulipwa:

1. Ligi ya NFL inawahitaji wachezaji wake wawe angalau wamemaliza shule ya upili miaka 3 nyuma. Hii huwasaidia kuhakikisha kuwa wachezaji hawa wamekomaa vya kutosha kushughulikia mahitaji ya kazi zao uwanjani. Wachezaji wengi huhudhuria vyuo vikuu kama daraja la pili la mafunzo yao ya kandanda, ambapo wanapocheza kwa ushindani vyuoni huwasaidia wachezaji hawa kuunganisha na kujenga uzoefu wao wa soka.
2. Maskauti wa NFL huhudhuria michezo ya wale wa akademi ili kutathmini vipaji vinavyotarajiwa nyakati zijazo. Kabla ya kuhitimu, wanasoka wengine huchagua kuendeleza taaluma zao kwenye ligi ya NFL huku wengine wakichagua kukamilisha digrii zao kabla hawajachaguliwa kucheza kwenye timu wapendazo ambazo zitawalipa fedha.

Mwanasoka anapaswa kujizoesha mara kwa mara ili adumishe uimara wa mwili na wepesi ili acheze kabumbu la kulipwa. Mara kadhaa kwa siku, wanasoka wengi wa kulipwa hufanya mazoezi ya uzito na yale ya misuli na pumzi. Mbali na mazoezi ya viungo, ni muhimu kwa wao pia kufanya mazoezi ya nafasi zao uwanjani na namna ya kuzitumia nafasi zao wawapo uwanjani ili wachangie ushindi kwenye michezo na kuzisaidia timu zao. Wachezaji wengi wa soka wanafanya mazoezi kwenye umri mdogo kwa sababu vyuo vingi na shule za upili huajiri wachezaji wanaoonesha kufanya mazoezi kwa bidii zaidi uwanjani.

Je, ni ujuzi wa aina gani ambao ni muhimu kwenye maisha ya kandanda? Sote tunaamini kwamba kufanya kazi kama mwanasoka wa kulipwa kunahitaji ujuzi wa viungo vyako ila upo ujuzi wa aina kadha wa kadha ambao unawawezesha wanasoka hawa wanaolipwa kuzisimamia taaluma zao na kushirikiana na wachezaji wenzao bila ya kujali nafasi zao kikosini:

  • Uratibu mzuri wa mambo;
  • Kufanya kazi kwa pamoja;
  • Uvumilivu;
  • Uimara;
  • Kasi;
  • Mkakati mzuri;
  • Nguvu ya kimwili;
  • Uelewa wa kujilinda uwanjani;
  • Kufanya maamuzi;
  • Kutunza muda;
  • Kukariri;
  • Maadili ya kazini.

Hitimisho

Kwa kuhitimisha, pale unapowashangilia wanakabumbu wako uwapendao au kuitazama michezo ya moja kwa moja kwa mshangao, kumbuka kuwa ulimwengu wa soka sio tu kuhusu shauku na utukufu wake – bali pia ni kuhusu mshahara wa mchezaji wa soka ambao anaupata. Hapa Parimatch, tunaamini kuwa kwa kushiriki kujua haya unakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi kuhusu ligi na wachezaji wa kuwabetia vyema.

Kama unajiona kuwa ni mwenye bahati na unataka kujaribu kusuka mkeka kwenye mechi za kandanda, basi tazama hapa Parimatch, jukwaa ambalo linajivunia uwepo wake wa kimataifa ulioimarishwa, unaojumuisha historia ya kuvutia ya kuwa na miaka 29. Jukwaa linatoa safu nyingi za michezo kwa wapenzi wa michezo ya kubashiri, hii inajumuisha e-sports na michezo ya vikatuni mtandaoni, na huwaruhusu watumiaji wawe na wepesi wa kuweka jamvi la kabla na wakati wa mechi za moja kwa moja.

Parimatch inajidhihirisha kwenye ubora wake, inayohitaji pesa kidogo sana, na hukuhakikishia michakato ya malipo ya haraka na ya kirafiki. Urahisi unaenea kwa kuwa na app ya simu, kuwezesha kuweka mikeka ukiwa mahali popote pale. Saa 24 za msaada kwa wateja, zinazopatikana kupitia gumzo la mtandaoni, WhatsApp, au barua pepe, huhakikisha unasaidiwa kila wakati unapohitaji iwe hivyo. Zaidi ya hayo, Parimatch huwavutia wachezaji kwa kuwa na aina mbalimbali za ofa na promosheni. Furahia mchezo, na timu bora itashinda!

Maswali Yanayoulizwa Sana

Mcheza soka anaingiza kiasi gani cha pesa kwa mwezi?

Kitaifa, wastani wa mshahara kwa wachezaji wa soka ni $2,706 kila mwezi.

Wacheza kandanda wanalipwa kiasi gani cha pesa kwa mwaka?

Kitaifa, wastani wa mshahara wa kwa wachezaji wa soka ni $32,476 kila mwaka.

Je, ni mwanasoka gani anayelipwa zaidi mwaka 2023?

Uhamisho wa kushangaza wa Neymar Jr kutoka klabu ya PSG kwenda Al Hilal ya Saudi Arabia umempandisha hadhi ya mchezaji kabumbu anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani, ana mshahara wa kushangaza wa dola milioni 240 kila mwaka, na anawapita wenzake kwa kiasi kikubwa hata kutoka kwa wale wanaocheza kwenye klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester United.

Wanasoka wa kulipwa wanalipwa kiasi gani kwa wiki?

Wanasoka bora zaidi nafasi ya mabeki wanaweza kutengeneza zaidi ya $576,923 hadi $480,769 kila wiki, ingawa mishahara ya mtu mmoja mmoja inatofautiana kulingana na uzoefu na uwezo wa kila mchezaji. Wachezaji wa ligi ya Championship pia hupata mapato zaidi, kwa wastani mchezaji hupata takriban $40,000 ikiwa ni mshahara wa wiki kwao kwenye ligi ya Championship.

Wachezaji wa Premier League wanalipwa pesa kiasi gani?

Wastani wa mshahara kwa wachezaji wa Premier League ni zaidi ya $60,000 kila wiki, ambayo ni sawa na zaidi ya dola milioni 3 kila mwaka. Wacheza soka wa Premier League ni miongoni mwa wanasoka wanaolipwa fedha nyingi zaidi kule nchini Uingereza.

Fahamu Zaidi:

YOUNG AFRICANS S.C.: UBABE WA KABUMBU LA TANZANIA
SIMBA S.C.: FAHARI YA WATANZANIA NA TIMU KUBWA YA SOKA LA AFRICA
SIMBA DHIDI YA YANGA: USHINDANI WA KIBABE KWENYE SOKA LA TANZANIA
SIMBA DHIDI YA AZAM: USHINDANI MKUBWA WA SOKA KWENYE UWANJA WA MICHEZO WA TANZANIA

Je, unahitaji kuwa wa kwanza kupata taarifa mbalimbali?

Subscription was successfully completed.