Wanacheza – Unashinda Jiunge sasa
Mwanzo / / Beti kwenye Hizi Timu 10 Bora za Kandanda Zilizofuzu AFCON 2024

Ni mara ya 34 ya mashindano ya kuvutia sana kwenye kandanda Africa, AFCON 2024 (Kombe la Mataifa ya Africa), limekaribia. Jumla ya timu 24 kutoka bara zima zitashiriki kwenye hii michuano wakiwania taji la ushindi.

Timu ya taifa ya Tanzania ya kabumbu, Taifa Stars, inakaribia kufanya mchujo wake wa 3, baada ya kukamata nafasi ya pili kwenye Kundi F kwenye mechi za kufuzu AFCON. Ukiachana nao kuna watabe wengine wa kandanda Africa, Morocco, Ivory Coast, Misri, Nigeria, Senegal, na kadhalika pia watashiriki.

Kwenye makala ijayo, nitakupa orodha ya timu 10 bora ambazo zimefanikiwa kufuzu kwenye Kombe la Mataifa ya Africa. Soma hapa twende pamoja na ujipatie uelewa mpana zaidi wa mashindano.

Je, ni timu gani zimefuzu kwenye Kombe la Mataifa ya Africa 2024?

Boigny Stadium of Abidjan

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa 2024 imepangwa kuanza Januari 13 na itaendelea mpaka Februari 11, 2024. Jumla ya viwanja 6 vya michezo kwenye miji 5 ya Ivory Coast kuchaguliwa kuandaa mechi zote. Hii ni pamoja na:

  • Dimba la Alassane Ouattara na dimba la Felix Houphouet Boigny, Abidjan
  • Stade de la Paix kule Bouaké
  • Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly huko Korhogo
  • Uwanja wa Laurent Pokou, San-Pédro
  • Uwanja wa Charles Konan Banny pale Yamoussoukro

Kama ilivyotajwa hapo awali, orodha ya timu 24 imekamilika kwa ajili ya hiyo michuano. Wakati Ivory Coast ikifuzu moja kwa moja kama wenyeji, timu 23 zilizosalia zilipata nafasi zao kupitia mchujo wa kawaida wa kufuzu.

Orodha kamili ya timu zote za Africa zitakazoshiriki AFCON 2024 ni hii hapa chini:

  1. Ivory Coast
  2. Morocco
  3. Algeria
  4. South Africa
  5. Senegal
  6. Burkina Faso
  7. Tunisia
  8. Egypt
  9. Zambia
  10. Equatorial Guinea
  11. Nigeria
  12. Guinea-Bissau
  13. Cape Verde
  14. Mali
  15. Guinea
  16. Ghana
  17. Angola
  18. Tanzania
  19. Mozambique
  20. Congo DR
  21. Mauritania
  22. Gambia
  23. Cameroon
  24. Namibia

Timu 10 Bora za Kombe la Mataifa Africa: Je, ni timu ipi itashinda?

Bila shaka timu zote 24 za Africa zinastahili kucheza kwa kiwango kikubwa kwenye droo ya mwisho. Hata hivyo, hakuna ubishi kuwa mbali ya kura, kuna timu chache zinazotarajiwa kufanya vizuri zaidi ya nyingine. Nimechagua kuelezea kwa undani timu kumi zinazotarajiwa kushinda Kombe la Mataifa Africa mwaka huu.

#1 Morocco (The Atlas Lions)

morocco football team(1)

Wa kwanza kwenye orodha hiyo ni Morocco, timu inayofanya vizuri zaidi kwenye soka la Africa kwa hivi sasa. Wameorodheshwa kwenye nafasi ya 11 duniani na wapo kwenye kampeni nzuri ya Kombe la Dunia la FIFA iliyofanyika Qatar. Timu ya Morocco, iliyojaa wachezaji wenye vipaji, ilitinga nusu fainali ya Kombe la Dunia lakini kwa bahati mbaya ikafungwa na Ufaransa kwa mabao 2-0.

Kwenye michuano ya AFCON, Morocco ipo Kundi F pamoja na DR Congo, Zambia, na Tanzania. Kwa kile ambacho kikosi kinaleta kwenye msimamo, kundi lililotolewa la Morocco ni rahisi sana kwa Achraf Hakimi, Hakim Ziyech, na kampani yao wote. 

#2 Senegal (Simba wa Teranga)

Kwenye namba mbili, ni timu ya FIFA iliyo kwenye nafasi ya 18 – Senegal. Ingawa Kombe la Dunia la FIFA la siku za karibuni ilikwenda kama ilivyotarajiwa kwa timu ya Kalidou Koulibaly, wamedhamiria kutwaa taji lao la pili la AFCON huu mwaka.

Wakizungumzia kuhusu droo yao kwenye Kombe la Mataifa ya Africa 2024, Senegal ipo kwenye kundi la Guinea pamoja na Cameroon na Gambia. Wamefuzu kama washindi wa Kundi L la raundi za mchujo.

Sadio Mané na wenzake wataanza kampeni yao hapo Januari 15 dhidi ya Gambia kwenye uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro.

#3 Tunisia (Eagles of Carthage)

Timu ya Tunisia inakamatia nafasi ya tatu kwenye orodha yangu ya timu 10 bora zitakazocheza AFCON 2024. Imeorodheshwa 28 kwenye orodha ya FIFA duniani, hii ni moja ya timu za Africa ambazo zimepata maendeleo makubwa kwa miaka ya hivi karibuni.

Imefuzu wakiwa kama washindi wa Kundi J, Tunisia inapata nafasi yake kwenye Kundi E la droo ya mwisho. The Eagles of Carthage wamepangwa pamoja na Mali, Namibia, na Africa Kusini, na mechi ya kwanza imepangwa kuchezwa mnamo tarehe 16 Januari.

#4 Algeria (The Desert Warriors)

Timu ya Taifa ya Soka ya Algeria, a.k .a. Mashujaa wa Jangwani wamepangwa kwenye orodha yangu pia. Mabingwa hao mara mbili wa AFCON (1990, 2019) wanakodolea macho mwaka mwingine wa kihistoria wakiwa na kikosi ambacho kinaonekana kuwa na matumaini kwenye karata zao uwanjani.

Washindi wa Kundi F wa raundi za mchujo wapo kwenye Kundi D la droo kuu pamoja na timu za Angola, Burkina Faso, na Mauritania. Huku mechi ya ufunguzi ikipangwa kupigwa mnamo tarehe 15 Januari 2024, Algeria ya Riyad Mahrez itatafuta mwanzo mzuri dhidi ya kikosi cha Angola.

#5 Misri (Mafarao)

Kwenye namba tano, nina kitu kwa ajili yako kuhusu timu iliyofanikiwa zaidi kwenye historia ya mashindano ya AFCON – Misri. Wanatambulika kwa jina la utani la Mafarao, Timu ya Taifa ya Misri kwa sasa ina mataji 7 kwenye makabati yao. Orodha ya mafanikio inaenda mbali zaidi na ushindi kwenye mashindano mengi makubwa, ikiwa ni pamoja na kombe la Waarabu la FIFA, michezo ya Kiarabu, michezo ya Africa, na zaidi.

Kuhusiana na AFCON 2024, Misri imepangwa kwenye kundi la Cape Verde ambalo pia linajumuisha nchi za Ghana na Msumbiji. Tazama mechi ya ufunguzi tarehe 14 Januari 2024 dhidi ya Msumbiji na ushuhudie Mohamed Salah akicheza kimaajabu sana.

#6 Nigeria (Super Eagles)

Timu ya Taifa ya Soka ya Nigeria (Super Eagles) imekuwa na msukumo sana kwenye kabumbu Africa. Kutoka kwenye kutoa wachezaji wa kiwango cha juu mpaka kushinda mashindano kwenye bara zima, timu imefika kileleni mara kadhaa. Inahusika kwenye nafasi ya juu zaidi ya FIFA ambayo ni ya 5 (iliyofikiwa mwezi Aprili 1994)

Kwa kushindwa kufuzu hivi majuzi kwenye Kombe la Dunia FIFA, timu ya Nigeria inalenga kurudi na taji la 4 la AFCON. Wakiwa wamepangwa kwenye Kundi A pamoja na Ivory Coast, Equatorial Guinea, na Guinea-Bissau, Super Eagles wataanza kampeni yao Januari 14.

#7 Cameroon (The Indomitable Lions)

Mabingwa mara 5 wa AFCON, Cameroon wanaingia kwenye toleo la 34 kama moja ya timu zinazopendelewa zaidi kushinda. Shukrani kwa kikosi chenye nyota wengi ambacho kina akina Darlin Yongwa, Frank Magri, Vincent Aboubakar, na wengineo, timu ya Rigobert Song imekuwa ni ya kipekee sana kwa siku za hivi karibuni. Inajumuisha kampeni kubwa ya kufuzu kwenye fainali za AFCON, ambapo waliibuka kuwa washindi wa Kundi C.

Kwenye droo kuu, Cameroon wapo kwenye Kundi C tena. Indomitable Lions itacheza dhidi ya Guinea, Gambia, na Senegal tarehe 15, 19 na 23 Januari hapo.

#8 Ivory Coast (Côte d’Ivoire/The Elephants)

Mwenyeji wa mabingwa wa AFCON 2024, Ivory Coast, pia yupo mbioni kunyakua taji lake la tatu la AFCON. Ingawa walikuwa ni wenyeji, timu ilifurahia kufuzu moja kwa moja; kamwe hauwezi kutilia shaka uwezo wa timu hiyo iwapo uwanjani. Ukizingatia mechi za mwaka 2024, kwa mfano, Côte d’Ivoire imepoteza alama mbili pekee kati ya mechi 11 ilizocheza. Hiyo inavutia mno!

Kwenye Kundi A lenye timu za Nigeria, Equatorial Guinea, na Guinea-Bissau, Ivory Coast inajivunia kuwa na kikosi imara. Kwa faida iliyoongezwa ya msaada wa ndani, haitashangaza kuona Ivory Coast ikinyanyua ubingwa pale dimbani.

#9 Burkina Faso (The Stallions)

Burkina Faso ni miongoni mwa timu za daraja la juu za Africa ambazo bado hazijashinda Ubingwa wa AFCON. Baada ya kuonesha uchezaji mzuri kwenye mechi za kufuzu, matumaini ni makubwa kuwa Bertrand Traoré na timu yake wataandika historia mwaka huu.

Lakini kwa ajili ya jambo hilo, Les Étalons inabidi kuzishinda timu za Algeria, Mauritania, na Angola kwenye hatua ya makundi. Timu ya taifa ya soka ya Burkina Faso itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Mauritania tarehe 16 Januari. Hii itafuatiwa na pambano la watabe zaidi wakiwa na Algeria mnamo tarehe 20 Januari.

Ratiba ya mwisho ya hatua ya makundi kwa timu ya Burkina Faso imepangwa kuwa ni Januari 23, 2024.

#10 Tanzania (Taifa Stars)

taifa stars

Sasa hatimaye, tuongee kidogo kuhusu Tanzania inayopendwa sana hapa nchini. Baada ya shoo kali kwenye hatua ya mchujo (wakiwa wabishi wa Kundi F), timu ya Taifa ya Tanzania imefanikiwa kuingia kwenye droo kuu ya AFCON kwa mara ya 3.

Kwenye kundi la Tanzania (ambalo ni Kundi F), utawakuta watabe wa Africa, Morocco, ambapo Taifa Stars watacheza nao mechi ya kwanza (tarehe 17 Januari). Mbali nao, timu nyingine mbili zinazoshika nafasi hiyo ni DR Congo na Zambia.

Bila shaka, ushindani utakuwa ni mgumu sana. Ila tukiwa na kikosi chenye vipaji, sote tunaweza angalau kutumainia utendaji mzuri wa timu hiyo. 

Wapi Pa Kubetia AFCON 2024?

Sasa kwa kuwa unafahamu kuhusu timu kuu za Kiafrica ambazo huenda zikashinda kwenye hiyo michuano ya bara, ni wakati wa kujadili mambo ya kupendeza kwa mashabiki wote. Itazame AFCON 2024 kwa kubeti na Parimatch—hii ni fursa yako ya kuwa zaidi ya mtazamaji tu!

Kwenye jukwaa hili, kubeti kwenye michezo huwa ni rahisi sana, na kandanda haina ubaguzi. Kama ungependa kufuata mbinu ya kiutamaduni ya kubeti kabla ya mechi kuanza au unapenda kubeti wakati mechi zikiwa zinacheza moja kwa moja, Parimatch huwa nawe wakati wote.

Kuanzia kutazama takwimu za mechi za ana kwa ana, na matokeo ya moja kwa moja mpaka kufikia msimamo wa hatua ya makundi na mengi zaidi, taarifa zote muhimu zipo mikononi mwako kila wakati. Unaweza kuzingatia haya, kuvinjari kwenye safu ya chaguzi za kubetia, na kubeti kwa hiari yako.

Kuongeza urahisi wa jambo hilo, Parimatch huwapa watumiaji wake app ya simu iliyoboreshwa vyema. Mimi nimejaribu mwenyewe, na inafanya kazi vizuri mno. Unaweza kuipakua kwa urahisi kwenye simu yako bila malipo na kuweka dau popote pale ulipo.

Utabiri wa AFCON 2024 na Dondoo za Kubeti

Ili utabiri matokeo ya Kombe la Mataifa Africa (AFCON), unatakiwa kuwa na mpango mahiri na uweke mikakati ya mikeka yako kadri ipasavyo. Kwanza, angalia namna kila timu inavyofanya kwenye michuano iliyopita ya AFCON. Tumia muda wako kuhakiki kile ambacho wanakifanya vizuri, ni wapi ambapo wanaweza kujipambania, na namna ambavyo wamekuwa thabiti.

Kisha, tazama aina ya sasa ya wachezaji wa muhimu na uone kama kuna ambaye ana majeraha yoyote, amezuiwa kucheza, au uchezaji bora ambao unaweza kuathiri nafasi za timu husika. 

Kwa mbinu ya kina zaidi, unaweza kuona namna timu zilivyofanya kwenye hatua ya raundi za kufuzu. Chunguza kwa ukaribu kama walifanya vizuri huko. Kasi hiyo inaweza kuwa ni sababu kubwa ya kuipeleka nchi au timu mbele kwenye hiyo michuano.

Hii inakuchosha? Shikilia jambo moja, kuna njia mbadala inayofaa kwenye hilo jambo. Kama wewe ni mtu ambaye unatafuta mbinu inayoendeshwa na taarifa zaidi lakini unahitaji muda zaidi wa utafiti wa kina, kutumia AI kwenye utabiri wako kunaweza kuwa ni jambo bora sana. 

Je, Ni Nani Anayetabiriwa Kuwania Kombe la Mataifa Africa 2024?

AI inasema kwa kuzingatia msimamo wa sasa na kwenye mchujo, Nigeria, Burkina Faso, Algeria, Mali, Morocco, na Senegal ndizo timu zinazotarajiwa kushinda mashindano hayo.

Je, unahitaji maarifa zaidi? Angalia kwa kina hii makala kuhusu utabiri wa kandanda wa AI.

Shinda AFCON 2024 Parimatch kwa Kutumia Timu Uipendayo

Hilo linahitimisha muongozo wetu kuhusu timu 10 bora za kandanda ambazo zilifuzu Kombe la Mataifa Africa. Kama umefuata kwa umakini, sasa unaelewa vyema tukio hilo ikilinganishwa na mashabiki wengi. Zaidi ya hayo, umevijua vidokezo vya ndani vya kufanikisha mikeka kwenye AFCON 2024. Kwa hiyo, kwanini usubiri? Tumia taarifa hii muhimu kupata ushindi kwenye michuano ya AFCON ukiwa na timu unayoipenda sana.

Kumbuka, Parimatch yuoo hapa kila wakati ili kufanya ubeti kwa urahisi. Pamoja na kuwa na manufaa ya kawaida kama vile maktaba pana sana, uwezekano wa kushindana, na kadhalika ukiwa kama mtumiaji, unaweza kufurahia bonasi za ushindi ulioboreshwa na msaada kwa wateja 24/7 uone yanayoendelea moja kwa moja. Fungua akaunti yako leo na uwe bingwa unayefuatia kwenye kubetia mechi za AFCON!

Maswali Yanayoulizwa Sana

Nani atakuwa mwenyeji wa Kombe la Africa 2024?

Ivory Coast inatazamiwa kuwa ndiye mwenyeji wa michuano ya 34 ya Kombe la Mataifa Africa. Michuano hiyo itafanyika kwenye viwanja 6 vilivyoenea kwenye miji mitano ya taifa.

Nani ameshinda zaidi Kombe la Mataifa Africa?

Misri ndiyo timu iliyofanikiwa zaidi kwenye historia ya michuano ya AFCON. Kufikia mwaka 2024, timu hiyo ina mataji saba kabatini mwake.

Ni timu ngapi zilizofuzu AFCON?

Jumla ya timu 24 zimefuzu kucheza AFCON mwaka 2024.

Je, Misri ilifuzu kuingia AFCON 2024?

Ndiyo, Misri imefuzu kuingia kwenye michuano ya AFCON 2024 wakiwa kama washindi wa Kundi D kwenye mchujo.

Je, unahitaji kuwa wa kwanza kupata taarifa mbalimbali?

Subscription was successfully completed.