Wanacheza – Unashinda Jiunge sasa
Mwanzo / / Viwanja 10 Bora vya Kabumbu Duniani (2024)

Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa zaidi nchini Tanzania na ulimwenguni kote. Kila wiki, mamilioni ya Watanzania hutazama timu na wachezaji wawapendao. Kuna sababu tofauti za kwanini mpira wa miguu unafurahisha sana. Kuanzia magoli ya ajabu na ujuzi wa mchezaji hadi matukio na kumbukumbu za ajabu, hisia hizo hazilinganishwi.

Ila baada ya muda, baadhi ya viwanja vimeonekana kuwa ni vya kipekee zaidi kuliko vingine, na hapa, tutachunguza viwanja kumi bora zaidi kwenye dunia ya kandanda leo. Kwa bahati nzuri, si lazima uwe kwenye uwanja wa klabu yako uipendayo ili uweze kuhisi msisimko wa kushinda. Ukiwa na Parimatch, unaweza kufurahia uwezekano bora na chaguzi bora zaidi za soko kwenye ligi zako zote uzipendazo, weka mkeka wako na ushinde. Tembelea tovuti yetu ili kuanza mchakato huo.

Ni Nini Kinafanya Uwanja Uwe Bora kwa Ajili ya Kandanda Duniani?

Kuna mambo mengi sana yanayojitokeza wakati wa kuainisha hadhi ya taswira ya uwanja. Umri wake, uwezo wake, historia/wakati na eneo. Tumezingatia mambo haya yote na zaidi, na tumeandaa orodha ya viwanja bora kumi ulimwenguni kwa upande wa soka. Hapa kuna orodha yetu:

#

Klabu Mahali Wamiliki Uwezo (Watu)

Mwaka

1

Wembley London, Uingereza Timu ya Taifa ya Uingereza 90,000 2007

2

Santiago Bernabeu Madrid, Hispania Real Madrid 81,044

1947

3

Camp Nou Barcelona, ​​Hispania Barcelona 99,354

1957

4

San Siro Milan, Italia A.C Milan, Inter Milan 80,018

1926

5

Old Trafford Manchester, Uingereza Manchester United 74,310

1910

6

Allianz Arena Munich, Uingereza Bayern Munich, Timu ya Taifa ya Ujerumani 75,024 2005
7 Anfield Liverpool, Uingereza Liverpool 53,394

1884

8

Bombonera Buenos Aires, Argentina Boca Juniors 54,000 1940
9 Maracana Rio de Janeiro, Brazil Flamengo, Fluminense 78,838

1950

10 Uwanja wa Kimataifa wa Cairo Cairo, Misri Al Ahly 75,000

1960

Viwanja Maarufu Ulimwenguni: Nafasi Kamili

Hivi ndivyo viwanja kumi vinavyovutia zaidi kwenye dunia ya soka hivi leo:

1 – Wembley

Wembley stadium

 • Mahali: London, Uingereza
 • Wamiliki: timu ya taifa ya soka ya Uingereza
 • Uwezo wa watu: 90,000
 • Mwaka wa kufunguliwa: 2007

Upo ndani ya moyo na nyumba ya soka, Wembley ni mojawapo ya viwanja vya kuvutia zaidi kwenye ulimwengu wa kabumbu. Uwanja huo ulifunguliwa kwa umma mnamo mwaka 2007 baada ya kubomolewa kwa uwanja wa zamani wa Wembley wenye umri wa miaka 101, na ukiwa na uwezo wa kuchukua watu 90,000, kwa sasa ndio.uwanja mkubwa wa mchezo wa mpira wa miguu nchini Uingereza na wa pili kwa ukubwa barani Ulaya.

Wembley ni nyumba ya timu za kitaifa za wanaume na wanawake za Kiingereza lakini pia huandaa mashindano mengine makubwa ya Uingereza kama fainali za Kombe la FA, Carabao au Kombe la Ligi, Kombe la FA, Ngao ya Jamii ya FA, na Vase ya FA. Pia, unaandaa mechi za mchujo kwenye ligi mbalimbali za kandanda huko Uingereza na Ligi za Kitaifa.

Uwanja huo wenye makao yake mjini London unachukuliwa kuwa ni mojawapo ya viwanja bora vya kabumbu ulimwenguni na umehusisha michezo ya kipekee kama vile fainali ya Ligi ya Mabingwa 2011 na fainali ya UEFA Euro 2020 ambayo iliifanya Uingereza kukosa mikwaju ya penati kwa Italia. Wembley pia itaandaa fainali ya UEFA Champions League 2024, ikiwa ni mara yake ya tatu na ya kwanza kwenye kipindi cha muongo mmoja. Pamoja na matukio mengine mengi ya kifahari yaliyopangwa, hakuna shaka kuwa ni uwanja bora nchini Uingereza.

2 – Santiago Bernabeu

Santiago Bernabeu stadium

 • Mahali: Madrid, Hispania
 • Wamiliki: Real Madrid
 • Uwezo wa watu: 81,044
 • Mwaka wa kufunguliwa: 1947

Kwa miongo mingi, Real Madrid imedumisha sifa yake kama moja ya vilabu vya hadhi ya juu ya soka duniani. Ni timu ya Ulaya iliyofanikiwa zaidi duniani na kwa urahisi kuwa ni maarufu zaidi kwenye soka. Miongoni mwa mambo mengi ambayo yamechangia mafanikio yao, Santiago Bernabeu ni mojawapo.

Uwanja huo uliopewa jina la mchezaji mashuhuri na rais wa klabu hiyo, Santiago Bernabeu Yeste, uwanja huo ulifunguliwa mwaka 1947 na ukawa ishara ya utambulisho wa klabu hiyo kwenye zama za baada ya vita. Kwa miaka mingi, imeshuhudia matukio mengi ya ajabu kama fainali ya Kombe la Ulaya la mwaka 1960 ambapo Ferenc Puskas na Alfredo Di Stefano walifunga magoli saba kwa pamoja na kuiwekea kando Frankfurt, goli la kukumbukwa la Hand of God la Diego Maradona katika fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 1986. na hatitriki ya Cristiano Ronaldo dhidi ya wapinzani wao, Atletico Madrid ambayo iliihakikishia Madrid nafasi na kutinga fainali. Uwanja huo pia umekuwa ni nyumba ya baadhi ya nyota wa kandanda ulimwenguni, kama Ferenc Puskas, Alfredo Di Stefano, Cristiano Ronaldo, Luis Figo, na Zinedine Zidane.

3 – Camp Nou

Camp Nou stadium

 • Mahali: Barcelona, ​​Hispania
 • Wamiliki: Barcelona
 • Uwezo wa watu: 1957
 • Mwaka wa kufunguliwa: 99,354

Camp Nou ni mojawapo ya viwanja bora duniani na lile linalotia hofu moyoni mwa mpinzani wao yeyote. Ni nyumba ya nguli wa FC Barcelona, ​​Camp Nou na ndio uwanja mkubwa wa mpira wa miguu kule Ulaya na moja ya uwanja wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kubeba watu zaidi ulimwenguni. Ulifunguliwa mnamo mwaka 1956 na umeshuhudia nyakati nyingi za kitabia katika kipindi cha historia yake ya miaka 67. Enzi ya miaka ya 1990 ilishuhudia Camp Nou ikikaribisha mojawapo ya timu kubwa zaidi za soka katika historia; Dream Team iliyoangazia magwiji wa muda wote kama vile kiungo mahiri, Pep Guardiola, mshambuliaji hatari, Romario, gwiji wa Uholanzi, Ronald Koeman, na mchezaji mwenye kipawa cha juu, Micheal Laudrup. Timu hii ilishinda mataji manne mfululizo ya La Liga na Kombe la Ulaya mnamo mwaka 1992.

Camp Nou pia imeona nyakati kadhaa za kushangaza ambazo zimeimarisha hadhi yake kama ngome. Mojawapo ni ule wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League 2016 dhidi ya PSG, ambapo Barcelona walishinda magoli 4-0 katika mchezo wa kwanza na kushinda 6-1 katika mchezo ambao sasa unaitwa La Remontada. Magwiji waliotamba kwenye uwanja huo ni pamoja na Lionel Messi, Ronaldinho na Romario.

4 – San Siro

San Siro stadium

 • Mahali: Milan, Italia
 • Wamiliki: A.C. Milan na Inter Milan
 • Uwezo wa watu: 75,817
 • Mwaka wa kufunguliwa: 1926

Ni viwanja vichache tu vya kabumbu duniani vinavyoweza kujivunia historia yenye utajiri ya San Siro. Ni nyumba ya vilabu viwili vilivyo na mafanikio zaidi katika soka (AC Milan na Inter Milan), San Siro ilifunguliwa mnamo mwaka 1926 na hapo awali ilitumiwa na A.C. Milan lakini baadaye ilifunguliwa kwa vilabu kwenye Manispaa ya Milan mnamo mwaka 1935. San Siro ilibadilishwa jina. Stadio Giuseppe Meazza mnamo mwaka 1980 kwa heshima ya mshambuliaji maarufu wa Italia ambaye alishinda Kombe la Dunia mara mbili na mataji mengi ya vilabu vya nyumbani akichezea vilabu vyote viwili.

San Siro imekuwa ni mwenyeji wa mechi za kukumbukwa za soka katika kipindi cha historia yake, ikiwa ni pamoja na sherehe za ufunguzi na mchezo wa Kombe la Dunia la 1990 na fainali za Ligi ya Mabingwa 2001 na 2016. Imekuwa pia ni nyumba ya hadithi kama Franco Baresi, Thiago Silva, Paolo Maldini, na Giuseppe Meazza.

5 – Old Trafford

Old Trafford stadium

 • Mahali: Manchester, Uingereza
 • Wamiliki: Manchester United
 • Uwezo wa watu: 74,310
 • Mwaka wa kufunguliwa: 1910

Old Trafford inaweza kuwa imeshuka katika suala la ubora na matengenezo katika miaka ya hivi karibuni, lakini hakuna kukataa historia yenye utajiri ambayo uwanja huo unaishikilia. Ni ya pili kwa kuwa ni uwanja mkubwa wa mpira wa miguu nchini Uingereza nyuma ya Wembley pekee na ni nyumba ya timu yenye hadhi kubwa nchini humo, Manchester United.

Uwanja huo umeona enzi nyingi za ajabu, kama enzi za Sir Matt Busby, ambazo zilishuhudia timu ikishinda mataji mengi ya ligi na Kombe la Ulaya. Enzi za Sir Alex Ferguson pia zilikuja na wimbi kubwa la mafanikio lililopelekea Manchester United kujulikana kama klabu kubwa zaidi katika kabumbu la Uingereza. Uwanja huo unaochukua watu 74,310 umepewa jina la utani la Theatre of Dreams, kama vile shuti la aina ya kibaiskeli la treble la mwaka 1999 lililopigwa na Rooney ambalo liliisaidia Manchester United kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza mwaka 2011.

6 – Allianz Arena

Allianz Arena venue

 • Mahali: Munich, Ujerumani
 • Wamiliki: Bayern Munich, Timu ya Taifa ya Soka ya Ujerumani
 • Uwezo wa watu: 75,024
 • Mwaka wa kufunguliwa: 2005

Uwanja wa Allianz Arena unaweza usiwe wa zamani kama viwanja vingine kwenye orodha yetu, lakini umejidhihirisha kama msingi wa soka la kisasa kutokana na nyota na nyakati ambazo umekuwa ni mwenyeji wa michuano. Ni nyumba ya wababe wa Ujerumani, Bayern Munich, Allianz Arena ndio uwanja wa pili kwa ukubwa nchini, na paneli zake za nje za plastiki za TFE zinazobadilisha rangi zinaufanya kuwa moja ya viwanja vya kupendeza zaidi duniani.

Uwanja huo umeshuhudia Bayern Munich ikishinda mataji kumi mfululizo ya Bundesliga na mwaka 2012 ilishuhudia Chelsea ya Uingereza ikichapwa na Bayern Munich na kushinda taji lao la kwanza kabisa la Ulaya.

7 – Anfield

Anfield football arena

 • Mahali: Liverpool, Uingereza
 • Wamiliki: Liverpool
 • Uwezo wa watu: 53,395
 • Mwaka wa kufunguliwa: 1884

Safari ya kwenda Anfield inaogopwa na takriban kila timu ya soka na mashabiki wa mechi. Anfield inachukuliwa kuwa mojawapo ya viwanja vya kutisha zaidi katika kandanda duniani, imekuwa na sehemu yake ya utukufu katika miongo kadhaa iliyopita. Licha ya kutokuwa moja ya viwanja vikubwa kwa uwezo, imebarikiwa na mashabiki ambao huandaa mazingira yasiyoweza kuvumilika kwa wapinzani.

Kumekuwa na nyakati nzuri kama vile ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Barcelona kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa 2019 na nyingine ambazo sio nzuri kama vile ‘kuteleza kwa Steven Gerrard’ na goli la Demba Ba ambalo liliigharimu Liverpool ubingwa wa Ligi Kuu ya mwaka 2014. .

8 – La Bombonera

La Bombonera football stadium

 • Mahali: Buenos Aires, Argentina
 • Wamiliki: Boca Juniors
 • Uwezo wa watu: 54,000
 • Mwaka wa kufunguliwa: 1940

Estadio Alberto J. Armando ni nyumba ya moja ya vilabu vikubwa zaidi vya nchini Argentina, Boca Juniors. Klabu iliyo na mashabiki wengi wanaofikia mamilioni na historia inayodumu kwa miongo kadhaa. Uwanja huo unaitwa La Bombonera kutokana na umbo lake lisilo la kawaida. Moja ya nguzo zake nne ni tambarare, huku nyingine tatu zikiwa na kina kirefu na muinuko.

Bombonera inamaanisha sanduku la chokoleti na inaelezea kikamilifu usanifu wa uwanja. Uwanja huo unajulikana kwa mazingira yake ya umeme, hasa katika michezo ya mashindano na River Plate. Pia, ulikuwa ni uwanja ambapo gwiji wa soka, Diego Maradona alicheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa na kufunga goli lake la kwanza katika maisha yake ya soka. Magwiji wengine waliowahi kucheza kwenye uwanja huo ni pamoja na Carlos Tevez, Roberto Mouzo, Juan Roman Riquelme, na Martin Palermo.

9 – Maracana

Maracana stadium

 • Mahali: Rio de Janeiro, Brazili
 • Wamiliki: Flamengo, Fluminense
 • Uwezo wa watu: 78,838
 • Mwaka wa kufunguliwa: 1950

Jumuiya ya wanasoka imeipongeza Brazil kwa kujitolea kwake katika mchezo na ukweli kuwa imezalisha vipaji vya kupendwa zaidi vya mchezo kama Pele, Ronaldo, Roberto Carlos, na Neymar, kwa hivyo haishangazi kwamba uwanja ambao umesheheni vipaji hivi na vingine kadhaa na ikafanya ari zaidi ya orodha yetu ya leo.

Maracanã ndio uwanja mkubwa zaidi nchini na wa tatu kwenye bara. Iliandaa fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 1959, mchezo ambao uliwaacha zaidi ya watu 200,000 katika mshtuko huku Uruguay ikiishinda Brazil na kushinda taji lao la pili, na pia kuandaa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014, ambapo Ujerumani iliishinda Argentina kwa goli moja. Pele alifunga goli lake la 1000 kwenye soka la Maracanã, na Neymar alifunga hatitriki yake maarufu ya mwaka 2014 dhidi ya Japan kwenye uwanja huo. Vipaji vingine vilivyotamba kwenye uwanja huo ni pamoja na Romario, Ronaldinho, na Garrincha.

10 – Uwanja wa Kimataifa wa Cairo

Cairo International Stadium

 • Mahali: Cairo, Misri
 • Wamiliki: Al Ahly
 • Uwezo wa watu: 75,000
 • Mwaka wa kufunguliwa: 1960

Ni nyumba ya klabu ya kabumbu yenye mafanikio zaidi barani Africa na mojawapo ya timu bora zaidi ulimwenguni, Al Ahly, bila shaka Uwanja wa Kimataifa wa Cairo ni moja ya viwanja bora vya kabumbu barani humo. Uwanja huo uliofunguliwa mwaka 1960, unaweza kuchukua watu 75,000 na umekuwa ni mwenyeji wa matukio ya kifahari kama fainali ya Kombe la Mataifa ya Africa ya 1986 na Kombe la Mataifa ya Africa 2006, ambapo Misri ilishinda.

Kutokana na mafanikio ya soka ya Al Ahly, Uwanja wa Kimataifa wa Cairo umejijengea heshima kubwa na kuwa uwanja bora wa kabumbu barani Africa. Al Ahly ni mojawapo ya timu za kabumbu zilizofanikiwa zaidi barani Africa na inaweza kuwa ni chaguo bora la kuibetia kama mdau wa michezo. Ili kuweka mkeka kwenye timu kutoka Tanzania, tembelea Parimatch. Tunatoa uwezekano bora zaidi, masoko ya kubashiri na bonasi kwa wachezaji. Pia, kuna app maalum ya simu ya mkononi na nafasi kwa wanaocheza kushiriki kwenye kubashiri moja kwa moja kwenye soka.

Muhtasari

Kwa hivyo una viwanja kumi maarufu zaidi kwenye dunia ya soka kwa leo. Viwanja hivi vilichaguliwa kwa kuzingatia historia na ushawishi wao kwenye ulimwengu wa soka na ilionesha jinsi uwanja unavyoweza kuwa muhimu kwa mafanikio ya nchi au ya klabu.

Kama shabiki wa soka wa Tanzania, wewe pia unaweza kuwa sehemu ya mafanikio haya, na hata bora zaidi, hauhitaji kutembelea uwanja unaoupenda ili kujionea! Unaweza kuonesha sapoti yako ukiwa umestarehe nyumbani kwako na bado ukatuzwa kwa kujisajili na kubeti mikeka yako. Ili kuanza, tembelea Parimatch leo ili kujisajili na kufikia uwezekano bora zaidi na chaguzi bora zaidi za kubashiri kwenye wachezaji bora, ligi na timu bora zaidi za kandanda duniani. Tembelea tovuti yetu kujisajili sasa!

Uwanja gani wa mpira wa miguu ni mkubwa zaidi?

Ukiwa na uwezo wa kuchukua watu 114,000, Uwanja wa Rungrado 1st of May ndio uwanja mkubwa zaidi wa soka duniani mpaka leo.

Ni uwanja gani wa mpira wa miguu una uwezo mkubwa zaidi?

Uwanja wa Rungrado 1st of May wa huko Korea Kaskazini ndio unaochukua nafasi kubwa zaidi ya kuwa na uwezo wa kubeba watu wengi kwenye kabumbu duniani hivi leo, lakini kwa upande wa viwanja vinavyotumika, Camp Nou, wenye uwezo wa kubeba mashabiki 99,354, unashika nafasi ya kwanza.

Ni uwanja gani wa mpira wa miguu ambao ni ghali zaidi?

Kwa makadirio ya gharama ya dola bilioni 1.57, uwanja wa Wembley wenye uwezo wa kuchukua watu 90,000 ndio uwanja wa soka ambao ni ghali zaidi katika historia. Viwanja kama vile uwanja wa Sofi na Yankee vinagharimu zaidi lakini kimsingi sio viwanja vya mpira.

Je, ni uwanja gani wa soka ulio bora zaidi duniani?

Santiago Bernabeu, Camp Nou, San Siro, na Wembley vinachukuliwa kuwa ni viwanja bora ulimwenguni.

Je, unahitaji kuwa wa kwanza kupata taarifa mbalimbali?

Subscription was successfully completed.