Mchezo bora wa esports, Dota 2 unapata umaarufu Afrika, na Tanzania haijaachwa. Lakini jinsi mchezo huu wa mtandaoni unavyo kua kiumaarufu, ndivyo jinsi kubeti Dota 2 kunavyo kua. Ndio maana Parimatch inakuletea mkusanyiko mpana wa machaguo ya kubeti Dota 2 na taarifa kadhaa juu ya jinsi ya kuanza.
Mchezo wa wachezaji wengi unaokwenda haraka, lengo la Dota 2 ni kubomoa gofu la maadui ndani ya ngome yao. Kuna tani ya njia za kushambulia ngome ya timu nyingine na kuwa mbunifu na mbinu yako ni nusu ya furaha.
Lakini si tu uchezaji mchezo wa Dota 2 ambao umekuwa pendwa Afrika nzima na Tanzania. Kubeti Dota 2 kumeenea sana na Parimatch iko kwenye usukani.
Kama wewe ni mpya kwenye ulimwengu wa kubeti esports, usiwe na wasiwasi, kiukweli ni rahisi sana kuelewa. Pamoja na utafiti kidogo, utakuwa mwalimu wa kubeti Dota 2 muda wowote.
Endelea kusoma kujifunza kuhusu mikeka tofauti Ya Dota 2, matukio maarufu zaidi ya kuyabetia, na maelekezo ya hatua kwa hatua juu ya jinsi ya kuweka mikeka kwenye Dota 2 kwa kutumia app ya simu ya mkononi na tovuti ya mtandaoni ya Parimatch.
Yaliyomo
Misingi ya Kubeti Dota 2
Kabla ya kwenda kwenye masuala ya msingi ya kubeti, ni muhimu kuwa na uelewa wa uchezaji wa mchezo wa Dota 2 na aina ya wahusika. Kama hauelewi jinsi mchezo huu unavyochezwa, huwezi kuweka mikeka sahihi.
Uchezaji wa mchezo
Dota 2 ni multiplayer online battle arena game, linalojulikana kivingine kama MOBA.
Sawia sana na majina kama League of Legends na CS:GO, kunakuwa na timu mbili ambazo zinapigana kukamilisha malengo fulani kabla ya mpinzani wao.
Timu zinakuwa na wachezaji 5, na kila mshindani anacheza kama moja ya madaraja 119 ya kipekee ya mhusika, au “mashujaa” kama wanavyojulikana katika huu mchezo.
Mechi huanza kwa kila timu kuanza kwenye pande tofauti za uwanja. Lengo la msingi ni kuwa timu ya kwanza kuharibu jengo kubwa lijulikanalo kama “Ancient” — ambalo linalindwa kwenye ngome ya timu pinzani.
Kuna aina zote za njia tofauti (au “lanes” kama zinavyojulikana katika mchezo huu) kufikia ngome ya mpinzani. Njiani, wachezaji hulenga kukamilisha malengo yasio ya upande wowote na kuua NPC’s (wahusika wasio wachezaji) ili kupata alama za uzoefu na rasilimali za thamani zilizotumika kumfanya shujaa wao kuwa mwenye nguvu zaidi.
Pindi moja kati ya timu inajiamini vya kutosha katika uwezo wao wa kishujaa, watashinikiza kuifikia “Ancient” ya timu nyingine. Kama wakifanikiwa katika jitihada zao, na kuweza kuharibu “Ancient” ya wapinzani, basi mchezo umeisha.
Aina za wahusika wa Dota 2
Sehemu ya kile kinachoifanya Dota 2 kuwa maarufu sana ni utofauti katika aina za wahusika. Kuna mashujaa 119 tofauti wa kuchagua, kila mmoja akiwa na uwezo wake mwenyewe wa kipekee.
Uwezo wa kishujaa unaotofautiana ni kiakisi cha majukumu yao maalum.
Kwa mfano, jukumu la shujaa mwenye sifa za juu sana za kujilinda lingeweza kusaidia kama chambo kwa timu pinzani — karibu kama ngao ya nyama. Wakati timu pinzani iko bize kushughulika na shujaa ambae ndo amevunja milango, ungeweza kuwa na shujaa mwingine anayetekeleza jukumu la kuwa mlengaji, kiusalama akipanga mashambulizi ya kuharibu kutokea mbali.
Pamoja na madaraja 119 ya mashujaa na mashujaa 5 tofauti kwenye kila timu, kuna kiwango kikubwa sana cha miunganiko. Hii pia humaanisha kuwa kuna mbinu nyingi sana tofauti ambazo timu zinaweza kupeleleza.
Aina za Mikeka Katika Dota 2
Sababu moja kwanini kubeti mtandaoni kwenye Dota 2 ni maarufu sana Afrika ni kwa sababu kuna machaguo mengi sana tofauti ya kuyabetia — na Parimatch ina yote ya hayo.
Mikeka ya moneyline
Unaweza kuwa tayari unaifahamu aina hii ya mikeka ya kitamaduni — ni babu wa mikeka yote. Unachagua tu timu gani unafikiri inakwenda kushinda. Ni hivyo.
Hivi ndivyo mikeka ya moneyline inavyoonekana kwenye Parimatch:
Kwa chaguo-msingi, Parimatch hutumia odds za desimali, lakini kwenye app yetu ya kubetia ya simu ya mkononi una chaguo la kuangalia odds katika mtindo wa fractional au American.
Kubeti kwa handicap kwenye Dota 2
Kubeti kwa handicap kunafanana na kubeti kwa moneyline, ni kwamba tu meneja ubashiri hutumia faida/hasara pepe kwenye timu kabla ya mechi kuanza. Odds zitachezeshwa kuakisi faida/hasara.
Hivi ndivyo aina ya handicap inavyoonekana kwenye Parimatch:
Hii ni mechi sawa kama mfano uliyopita. Tambua jinsi odds zinavyobadilika pindi handicap inapotumika.
Katika kesi ya Dota 2, handicap hutumika katika mtindo wa map lead kabla ya mechi kuanza. Hivyo katika mechi ya “bora kati ya 5”, Live to Win inaongoza kwa mizunguko 1.5 kabla hata shindano halijaanza.
Tuseme ulichagua Vikin.gg kushinda. Ili mikeka yako ilipe, wangepaswa kushinda mechi kwa walau mizunguko 2 katika mechi ya mzunguko wa “bora kati ya 5”.
Kama Viking.gg ingeshinda mechi kwa alama ya mizunguko 3 kwa 0, mikeka yako ingelipa kwa sababu wangeshinda kwa zaidi ya mizunguko 1.5.
Kama wangeshinda mechi kwa alama ya mizunguko 3 kwa 2, mikeka isingelipa kwa sababu wangeshinda mechi kwa mzunguko 1 tu.
Mikeka ya jumla kwenye Dota 2
Katika soko la jumla, unakuwa unaombwa kutabiri kama unafikiri “kitu fulani” kitatokea zaidi au pungufu (over/under) kuliko idadi ambayo meneja ubashiri anatoa. Katika Dota 2 hicho “kitu fulani” ni maps zinazohitajika kuchezewa kwa ajili ya mshindi.
Kumbuka, mechi za Dota 2 huchezwa katika mtindo wa “Bora kati ya”. Hivyo, katika soko la jumla la Dota 2, kimsingi unabetia kiasi gani cha muda unachofikiri mechi itadumu.
Huu hapa ni mfano kutoka kwenye sportsbook ya mtandaoni ya Parimatch:
Mfano huu unatoka kwenye mtindo wa staili ya maps ya “bora kati ya 3”. Unatakiwa kuamua kama unaamini mechi itakuwa imeisha baada ya maps 2 au, kama unafikiri timu zitagawana maps 2 za kwanza, katika map ya 3 ya muhimu na yenye maamuzi. Pindi umefanya utabiri huo, umepata mikeka yako.
Kubeti kwenye firsts katika Dota 2
Moja ya mikeka maarufu za Dota 2 ni kubeti kwenye firsts. Hii humaanisha unatakiwa kutabiri ipi kati ya timu itatimiza “kitu fulani” kwanza.
Kwa mfano, kwenye sportsbook ya mtandaoni ya Parimatch, una chaguo la kubeti kwenye timu gani unafikiri itapata uuaji wa kwanza (first blood). Kama hauipendelei aina hiyo, ungeweza kubeti kwenye timu gani unafikiri itateka mnara wa kwanza au timu gani unafikiri itaharibu kambi za kwanza.
Hizi hapa ni firsts zote unazoweza kubeti kwenye Dota 2:
Kuweka mikeka maalum ya Dota 2
Sehemu ya sababu kwanini kubeti Dota 2 ni maarufu sana Tanzania ni kwa sababu Parimatch hutoa mikeka fulani maalum inayovutia sana ambapo hutaweza kuzipata sehemu nyingine yoyote.
Mikeka maalum ni masoko ya kubeti ambayo ni ya kipekee kwa esport maalum.
Kwa mfano, taji pekee la esports ambapo timu inaweza kunyakua “Aegis of the Immortal” ni Dota 2, na Parimatch hukupa chaguo la kulibetia hilo.
Hii hapa ni mifano baadhi ya machaguo ya mikeka maalum ya Parimatch kwa ajili ya Dota 2:
Matukio Makubwa Zaidi ya Dota 2 ya Kuyabetia
Kubeti mtandaoni kwenye Dota 2 kunasisimua zaidi pindi unapobetia tukio kubwa. Baadhi ya mashindano makubwa zaidi hulipa jumla za pesa katika mamilioni. Pamoja na mengi sana kuwa hatarini, matukio haya makubwa zaidi yanaweza kuwa na mhemuko sana, ambacho huyafanya ya kuvutia sana kwa mtazamaji.
Matukio makubwa si tu yanasisimua zaidi kuyatazama, lakini pia kuna taarifa na uchambuzi mwingi zaidi juu ya timu. Hii hufanya kuwa rahisi zaidi kufanya utafiti wa kiutabiri na kuweka mikeka sahihi.
Dota Pro Circuit
Dota Pro Circuit ilitambulishwa 2017 na watengenezaji wa Dota 2, Valve. Shindano hili lilianzishwa kuamua timu zipi zinastahili kupata mwaliko wa moja kwa moja kwenye tukio kubwa la esports, The International.
Kuna idadi sawia ya timu kutoka Marekani Kaskazini, China, Ulaya, Asia Kusini Mashariki, Marekani Kusini, na Jumuiya ya Madola ya Maeneo ya Mataifa Huru.
Timu hizi hutuzwa alama za kufuzu kulingana na jinsi zinavyomaliza katika mashindano. Mwishoni mwa msimu, timu 12 bora hualikwa kwenye The International.
The International
Tukio la esports kubwa zaidi na lenye faida kubwa zaidi juu ya uso wa dunia ni The International.
Jumla yake ya pesa 2019 ilikuwa karibia dola milioni 35 na timu iliyoshinda ilikusanya juu kidogo ya dola milioni 15. Pamoja na aina hizi za namba, kwa hakika unaweza kuelewa kwanini inasisimua sana kutazama. Baadhi ya wachezaji hawa hutoka kwenye umaskini hadi utajiri ndani ya usiku mmoja na tukio hili hufanya kazi nzuri sana kuangazia stori zote.
The International ni kito cha taji la mandhari ya esports ya Dota 2. Kama uko makini kuhusu kubeti kwenye Dota 2, tukio hili uhitaji akili kidogo.
China Dota2 Pro Cup
China Dota2 Pro Cup huwa na timu za wataalamu za Dota 2 kutokea China. Kombe hili huangazia timu 10 ambazo zote zinashindania jumla ya pesa dola 80,000.
8 kati ya timu 10 hupokea mwaliko wa moja kwa moja na nafasi mbili zinazobakia zinatuzwa kwa timu kutokea shindano la wazi la kufuzu.
Shindano hili lina hatua ya makundi ikifuatiwa na michezo miwili ya marudiano ya mtoano na mechi zote zinachezwa katika mtindo wa map ya bora kati ya 3.
Hata kama shindano hili sio kubwa zaidi, bado linahusisha baadhi ya wachezaji wazuri zaidi wa Dota 2 ulimwenguni. Limekuwepo tu kwa mwaka na kama ukuaji mkubwa wa esports ukaashiria kuendelea, haitachukua muda mrefu kabla China Dota2 Pro Cup haijaupa upinzani umaarufu wa The International.
Jinsi ya kuweka mikeka kwenye Dota 2 kwenye Parimatch
1.Tembelea ukurasa wa nyumbani wa Parimatch
2. Juu kulia mwa skrini, chagua ingia au jisajili. Hivi ndivyo jinsi ya kusajili akaunti yako.
3. Baada ya kuingia, weka pesa katika akaunti yako.
4. Pindi umeweka pesa kwenye akaunti yako, nenda tena kwenye ukurasa wa nyumbani na bofya kwenye E-sport. Unaweza pia kuipata katika menyu ya “Sports”.
5. Chagua Dota 2 kutoka kwenye orodha ya esports zinazopatikana.
6. Chagua ligi au shindano unalotamani kulibetia kutoka kwenye menyu ya mdondoko wa chini.
7. Baada ya kuwa umechagua ligi/shindano gani la kulibetia, chagua mechi maalum unayotaka kuibetia.
8. Kinachofuata, pitia kutazama ukurasa na chagua aina yako ya mikeka unayotaka.
9. Baada ya kufanya chaguo lako, angalia kulia mwa skrini kwenye tiketi ya ubashiri na ingiza kiasi gani unataka kubetia.
10. Kama umeridhika na mikeka yako na uko tayari kuiweka, chagua “weka mikeka”.
11. Kuweka mikeka mingi, rudia hatua ya 4 mpaka ya 10.
12. Pindi uko tayari kuweka mikeka yako, nenda kwenye tiketi ya ubashiri.
13. Bofya “Parlay” kuweka mikeka ya parlay. Ongeza mikeka yako na bofya kuweka mikeka yako.
14. Bofya “System” kuweka mikeka ya system. Ongeza mikeka yako na chagua system ambayo ungependa kubeti nayo kutoka kwenye menyu ya mdondoko wa chini. Halafu bofya kuweka mikeka yako.
Dondoo za Kubeti kwenye Dota 2
Angalia takwimu
Weka umakini kwenye uchezaji wa kihistoria wa timu. Takwimu zitakupa ishara ya nini kila timu inakabiliana nacho. Kwa mfano, unaweza kuangalia kwenye mauaji ya wastani, dakika wastani, na maps wastani zilizochezwa kutoka kwenye mechi za Dota 2 zilizopita.
Taarifa zote hizi zitasaidia kama ishara ya nini cha kutarajia katika mashindano. Takwimu hizi zinapatikana kwa urahisi na haitakugharimu kitu. Hakikisha unafanya kazi yako, hakika itakusaidia kufanya tabiri zilizo sahihi zaidi.
Ondoa Mhemuko
Wabashiri wenye mafanikio zaidi duniani hujua kuwa hisia zao binafsi kuhusu timu hazimaanishi kitu inapokuja kwenye kuweka mikeka erevu kwenye Dota 2.
Hivyo ni kusema, muda mwingine unatakiwa kuiunga mkono timu usiyoipenda ili kujipa fursa nzuri zaidi ya kushinda.
Bila shaka, unataka kuiunga mkono timu yako pendwa, lakini hakikisha unabeti bila upendeleo wowote. Kumbuka, ni wewe dhidi ya meneja ubashiri, na mameneja ubashiri kwa hakika huwa hawafanyi kazi na chembe hata moja ya upendeleo.
Pata taarifa
Kipengele kimoja cha epsorts ambacho huifanya kuwa shirikishi sana ni jumuiya zao husika. Mashabiki katika jumuiya ya mtandaoni hupenda kuangalia mechi za Dota 2 na kushirikisha maoni yao.
Unaweza hata kuuliza swali maalum sana na ndani ya dakika ukapata tani ya mrejesho kutoka kwa mashabiki na wabashiri wa Dota 2 wenye mtazamo mmoja na wewe.
Hakika, utakutana na tabiri chache za kufedhehesha lakini utasoma pia hoja zenye nguvu na mawazo yenye msingi wa ukweli — ambavyo vinaweza kuwa na athari chanya kwenye tabiri zako mwenyewe.
Kuangalia mechi inayokuja kutoka kwenye mtazamo wa mtu mwingine hukusaidia kuweka mikeka iliyofikiriwa vizuri. Eti, unaweza hata kupata rafiki mpya.
Weka umakini kwenye habari
Timu za esports ni kama tu timu nyingine zozote za kitamaduni. Ni kundi la watu wanaokuja pamoja na wanajiandaa kwa ajili ya mechi halafu wanashindana.
Kama tu michezo ya kawaida wachezaji wanaweza kuondolewa, kuuzwa, kukopwa, au kubadilishwa nje ya kikosi kwa sababu nyingine kadhaa.
Hakikisha unafahamu habari za hivi karibuni ili uweze kuwa unajua mabadiliko yoyote ya dakika ya mwisho. Kitu kibaya zaidi unachoweza kufanya ni kuweka mikeka, kuja tu kujua kwamba mchezaji wao supastaa ambaye huwa anabadili mchezo yuko nje ana carpal tunnel syndrome (hii hutokea zaidi kuliko unavyoweza kufikiria).
LAN dhidi ya Mtandaoni
Baadhi ya mechi za esports zinachezwa mtandaoni — ambapo washindani wanaweza kuwa mbali kieneo kwa maelfu ya maili kutoka kila mmoja wakiwa wametulia kwenye nyumba zao wenyewe. Baadhi ya mechi kubwa zaidi zinachezwa kupitia LAN (mtandao wa eneo la karibu) katika uwanja mkubwa uliyojaa mashabiki wenye bashasha.
Fikiria kuhusu jinsi shinikizo la umati linavyoweza kuathiri utendaji wa washindani. Watafanya vizuri chini ya shinikizo hilo au watashindwa na kucheza chini ya kiwango?
Wengi kati ya wataalamu hawa walikuwa wakikaa kwenye makochi yao muda si mrefu uliyopita na kucheza kwenye uwanja uliyojaa kunaweza kuwa na shinikizo. Fahamu hali zinazoizunguka mechi maana zinaweza kuwa na athari kwenye matokeo.
Taarifa zaidi kuhusu Kuweka Dau kwenye Esports:
- Dondoo 7 Bora za Kubeti kwenye Esports
- Jinsi ya Kubeti kwenye Counter-Strike: Global Offensive!
- Jinsi ya Kubeti kwenye League of Legends
- Ligi ya SRL ni Nini – Muongozo Kutoka Parimatch
- Yote Yanayohusu Kasino ya Parimatch
- Shinda Kitita cha Pesa Unapocheza JetX Parimatch!
Hitimisho
Tasnia ya esports inakua sana sasa hivi Afrika na ni mwanzo tu. Ulifahamu kuwa tasnia ya michezo ya video tayari ina umiliki wa soko mkubwa zaidi kuliko tasnia za filamu na maigizo zikiunganishwa? Hiyo ni ajabu.
Kubeti mtandaoni kwenye Dota 2 ni njia ya kusisimua ya kujizamisha katika dhana hii ya kidunia ambayo ni esports. Usikose nafasi yako kuingia kwenye uchezaji.
Baada ya kusoma mwongozo huu, umeimarishwa na zana na maarifa yote ya muhimu kuanza kuweka mikeka ya ushindi na Parimatch.
Haijalishi mtindo wako unaoupendelea, Parimatch ina hakika kuwa na kile unachokitafuta. Nenda kwenye sportsbook yao ya mtandaoni na angali wewe mwenyewe!