Hapa Parimatch tumejizatiti kuwapa wateja wetu burudani kupitia michezo ya kubashiri, hii ni kwa wateja wetu wote barani Afrika, tunalenga kuwapa fursa ya kubeti kwenye michezo yote mikubwa dunaini kupitia app ya kubetia ya kisasa zaidi iliyotengenezewa kukidhi mahitaji yako yote.
Kuwapa wateja wetu fursa ya kufurahia kubeti kwenye machaguo mengi zaidi ya kubeti nchini Tanzania, tunawapa wateja wetu nafasi ya kufurahia odds kubwa na za kuvutia kwenye mechi nyingi kupita maelezo.
Kwa wale wanaotaka kubeti kisasa Parimatch ipo upande wako, Double chance ni moja ya mbinu nyinyi za kubetia na kukuwezesha kushinda na ni moja tu kati ya masoko yanayopatikana ndani ya Parimatch.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu kubetia Double chance, tumekuandalia maelezo kwenye makala hii kukupa mbinu zitakavokuwezesha kucheza na kushinda na Parimatch kupitia Double chance.
Yaliyomo
Tips za Kubetia Double Chance
Double chance ni mbinu nzuri ya kupunguza uwezekano wa kuchana mikeka yako na kukuongezea uwezekano na kushinda na kuondoka na mshiko wa kutosha, Double chance siyo mbinu nzuri tu ya kupunguza uwezekano wa kupoteza bali ni moja ya mbinu rahisi zaidi kujifunza na kuielewa, kabla ya kuanza, shika kwanza vitu hivi kichwani mwako:
- Double chance ndiyo mbinu bora zaidi ya kujiokoa na uwezekano wa kupoteza hela zako kwani hapa unabeti kwa matokeo mawili kwa mara moja
- Kwa kuwa ni rahisi sana kushinda mikeka ya Double chance kwa kuwa una nafasi mara mbili, hii inamaanisha pia faida yako itakuwa ndogo kwenye mikeka ya moneyline.
Double Chance ni Nini?
Kubeti kwa njia hii ni rahisi kama inavyojieleza yenyewe, ukiwa unaweka mkeka kwenye kubeti kwenye mashindano yoyote unakuwa na nafasi mara mbili ya kushinda, ni muhimu kuelewa kuwa japo una nafasi mara mbili ya kushinda, unapunguza nafasi ya odds zako na faida yako.
Inafanya kazi kiurahisi sana, fikiria mchezo wowote wenye matokeo matatu; timu A kushinda, timu B kushinda na matokeo kuwa ya sare, Double chance inakuwezesha kwenye matokeo mawili unayoamini yana uwezekano mkubwa wa kutokea, kwa mfano unaweza kubeti timu A itashinda na kutoa sare au unaweza kubeti timu B itashinda au kutoa sare kwenye mchezo husika.
Tuchukue mfano wa uhalisia kwenye mchezo huu ambao tunauona kati ya Wolverhampton Wanderers (Wolves) na Aston Villa (Villa):
1 or Draw | 1.22 | No draw | 1.27 | 2 or Draw | 1.81 |
Wolves inawakilishwa na ‘’1’’ na Villa kwa ‘’2’’ . Unaweza kubetia kwa kuchagua Wolves kushinda au kutoa sare. Unaweza kubashiri pia Wolves na Villa kushinda bila kuwa na droo. Au mwisho kabisa unaweza kubetia Aston Villa kushinda au kutoa sare.
Kwa wale waliobeti kwa wolves kushinda au kutoa sare (“1 or Draw”), odds zake in 1.22. Hii inamaanisha ukibetia TZs 50,000 na Wolves wakashinda, utapata TZs 61,000 — na faida ya TZs 11,000. Kama Wolves watapata sare basi hii itabakia hivihivi, na kama Villa utapoteza TZs 50,000 ya dau lako
Ukibeti kwa Wolves au Villa kushinda, unakuwa unabeti kwamba hakutakuwa na Draw kwenye mchezo huu. 0dds zake zitakuwa 1.27, maana yake utapata faida ya TZs 13,500 endapo mchezo hautaisha kwa sare
Kwa urahisi zaidi kama Villa atashinda au kupata sare kutawawezesha waliobeti kushinda na kupata faida kubwa ya TZs 40,500 kwa dau la TZs 50,000.
Masoko ya Kubeti kwa Double Chance Ukibeti na Parimatch
Parimatch inawazawadia wateja wake fursa ya kubeti kwenye masoko kibao, kwenye timu za soka na kwenye michezo mingine kibao, kwa mikeka ya Double chance, ni moja ya chaguzi nyingi kwenye jukwaa la Parimatch, uwepo wa Double chance unatuwezesha kuwapa fursa wateja wetu kubeti kwenye michezo mingi kadri wawezavyo ndani ya Parimatch, siyo hivyo tu, bali tunaruhusu Double chance kwenye michezo ya live na michezo ya virtual.
Ni michezo gani unayoweza kucheza Double chance ndani ya Parimatch.
Moja ya vitu vya kuvutia zaidi kucheza na Parimatch ni jinsi ilivyo rahisi kutumia mfumo, kwa wale wanaohitaji kucheza kwa kutumia Double chance, ni rahisi kutembelea app ya Parimatch na kutimiza lengo lako kiurahisi kabisa.
Haijalishi ni mchezo gani ambao unataka kuucheza, Parimatch inakupatia options rahisi za Double chance, wewe ni shabiki wa ice hockey? Kwanini usiweke mkeka wako wa Double chance kwenye NHL?
Labda wewe ni shabiki wa soka? Usijali kuna michezo kibao ya soka ya kucheza Double chance.
Pengine labda wewe ni shabiki wa michezo ya kishua zaidi kama rugby. Cheza Double chance kwa kujidai kabisa kwenye mashindano ya English Rugby Union Premiership ukiwa na Parimatch.
Mbadala, kwanini usijaribu kubetia Double chance kwenye mashindano ya kibabe zaidi barani Ulaya ya handball?
Weka mkeka kabla ya mechi, live na cheza Double chance kwenye michezo ya virtual
Parimatch ni mfumo unaomuwezesha shabiki wa soka wa karne ya 21 kucheza na kujihusisha na michezo mbalimbali ndani ya jukwaa moja, kuweka mkeka kidigitali kunamaanisha unaweza kufurahia kucheza na Parimatch ukiwa mahali popote, hakuna haja ya kupanga foleni kwenye maduka, Parimatch inakupatia kila kitu unachohitaji kubetia kwenye mchezo wowote. Utofauti mkubwa kwa Parimatch ni kwamba kila kitu kipo, kazi yote inabakia kwako kufanya maamuzi ya unataka kushinda wapi? Iwe ni live au kabla ya mechi, tupo kwa ajili yako.
Kwa wale wanaopenda mzuka, kucheza Double chance mchezo ukiwa live kutakupa msisimko wa tofauti kabisa, tofauti kubwa ya kubeti Double chance mchezo ukiwa live na kucheza kabla ya mchezo kuanza ni ukubwa wa odds, ukicheza mchezo ukiwa live odds zitapungua na kuongezeka kutokana na matukio yanayoendelea ndani ya mchezo lakini ukicheza kabla ya mchezo kuanza mara nyingi odds hazibadiliki. Ukitaka kucheza live kwenye app yetu ya kisasa bofya kitufe cha cheza “Live”.
Endapo hautatosheka kubetia kwa Double chance kwenye michezo mbalimbali, app yetu ya kisasa inakupatia fursa ya kubetia kwenye michezo ya virtual, ingia kwenye ulimwengu wa virtual na uweke mkeka wako wa Double chance bila ya kuwa na haja ya kusubiri mchezo wenyewe, tembelea kwenye eneo lililoandikwa “Virtual” kwenye app ya Parimatch kupata nafasi ya kucheza Double chance.
Kwanini watu wanacheza Double chance?
Kubeti kabla ya mechi kunakuwezesha kufanya ubashiri wa mchezo husika kabla haujaanza, sahau kuhusu mkeka kisha sikilizia matokeo ya mechi ujue kama umeshinda au lah.
Kubeti live ni tofauti kidogo, japo ni aina ya mikeka yenye mzuka wa aina yake, ukiwa unabeti live, unatumia hali halisi ya mchezo husika kubashiri namna ya kuweka mikeka yako. Kama michezo ya live inavyoendelea na matukio kubadilika, lakini ndivyo ilivyo kwa odds za live, nazo hubadilika kila muda.
Kwa mfano, fikiria kipa wa timu A ametolewa nje kwa kadi nyekundu ndani ya kipindi cha kwanza, odds za Double chance kwa timu A kushinda au kutoa sare zitaongezeka maradufu, kwa kuwa uwezekanao wa timu A kushinda unakuwa umepungua mno hapo, kwa wale walioweka mkeka wa ushindi kwa timu A kabla ya mechi kuanza, hawatafaidika na kubadilika huku kwa odds endapo timu A itashinda kwa miujiza.
Jinsi ya kuweka mkeka wa Double chance ukiwa na Parimatch
Parimatch ikijiamini kwa kuwa na app bora zaidi ya michezo ya kubashiri barani Afrika, kila kitu kipindi cha kuundwa kwake kinazingatia uhitaji wa mtumiaji na kutengezwa kuhakikisha hata mtu ambaye hana uzoefu na teknolojia anatumia kwa urahisi.
Haya hapa ni maelezo ya hatua kwa hatua ya kucheza na kushinda kwenye Double chance ukiwa na Parimatch:
- Kwanza kabisa, kama hauna akaunti ya kubeti ya Parimatch, itakubidi ufungua akaunti mpya mara moja, utahitajika kusign up, unaweza kwa kuanza kujisajili kwa kwenda kwenye app ya Parimatch au kwenye tovuti. Kisha bofya kitufe cha “Sign up”.
- Ukishamaliza kujisajili na kuweka deposits, unakuwa upo tayari kutengeneza Double chance ndani ya Parimatch.
- Bofya kitufe cha “Sport” kwenye menyu, hii itakusaidia kuingia kwenye kurasa ambayo ina michezo yote unayotaka kuibetia.
- Baada ya kuchagua mchezo utaona nchi zote ambazo mchezo huo unapatikana, orodha hii ndefu inathibitisha ni kwa jinsi gani Parimatch wamejizatiti kukupatia chaguzi zote unazozitaka.
- Chagua nchi ambayo mchezo unaoutaka unapatikana kisha baada ya hapo chagua ni mashindano gani mchezo huo upo kabla ya kuweza kubetia.
- Bofya kuchagua cup, championship, au league ambayo utahitaji kuweka mkeka wako wa Double chance.
- Chagua mechi unayotaka kuweka mkeka wako. Ukibofya itakupeleka kwenye ukurasa wa kubetia, kamilisha kwa chaguzi unazozitaka.
- Baada ya kuchagua mikeka yako nenda kwenye Bestslip yako kukamilisha mkeka Wako.
- Unaweza kuchagua hii parlay kama una timu zako za kutosha.
- Angalia mkeka wako wote kisha shuka chini kwenye kitufe cha “Weka mkeka”.
Faida za Kubetia Double Chance
Faida ya kwanza na kubwa zaidi ya kucheza Double chance ni kwamba uwezekano wa kushinda unaongezeka maradufu, kukiwa na matokeo matatu kwenye kila mchezo, ukicheza Double chance unakuwa umechagua matokeo mawili hivyo uwezekano wa wewe kushinda kwa kuchagua matokeo matatu unaongezeka zaidi.
Hii inaifanya Double chance kuwa moja ya mbinu rahisi zaidi za kubeti na kushinda, njia rahisi ya watu wanaoanza kucheza au kujifunza kubeti ni hii.
Wataalamu wa kubeti wanajua kutumia Double chance kwa timu ndogo, fikiria Man U inacheza mchezo wa UEFA Champions Cup, Jumatatu, lakini wikiendi hiyo hiyo Man U wanacheza na Wolves, hivyo kulinda wachezaji kwa ajili ya UEFA, Man U watachezesha wachezaji wadogo kulinda kikosi chao, watalaamu wanatumia nafasi hii, kubeti Double chance kwa Wolves kushinda na kuondoka na ushindi ni mkeka wa uhakika.
Hasara za Kucheza Double Chance
Hasara kubwa ya kubetia Double chance ni kwamba odds zake zipo chini sana, kwa kuwa unakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kushinda kuliko kucheza na kubetia kwenye mikeka ya kawaida, odds za timu yenye uwezekano mkubwa zaidi wa kushinda ni ndogo zaidi kuliko kwenye timu ambayo haipewi nafasi ya kushinda.
Faida za Kucheza Double Chance na Parimatch
Tukiwa na jukwaa kali zaidi la kubeti barani Afrika, Parimatch inajigamba kwa kuwa na huduma za kipekee na app bora kuliko zote.
- App rafiki kwa mtumiaji
Parimatch imetengeneza app kali mno kwa watumiaji wa vifaa vyote vya Android/iOS ambayo inawawezesha watumiaji na wateja kubeti kwenye mechi na michuano mbalimbali duniani kote, ikiwa imeundwa kwa kumfikiria mteja na uhitaji wake, hivyo ni rahisi sana hata kwa watu wanaojifunza. Rahisi sana kupakua huku ukiweza kuweka pesa na kubeti chap chap tu.
- Wingi wa michezo ya kucheza Double chance
Parimatch imejizatiti kuwaletea wateja wake michezo mingi na nafasi kubwa ya kuchagua ni aina gani ya michezo, michuano na timu gani unazotaka kubetia, utakuta ofa yako ya kucheza Double chance kwenye michezo kibao kuanzia handball hadi soka na hockey, Parimatch inakuruhusu kuweka Double chance kwenye michezo yote hii.
- Beti Double chance 24/7
Jukwaa letu la kubeti limetengenezwa kwa namna ambayo mteja anapata michezo anayotaka kubetia muda wote na wakati wote, tunatoa huduma za wewe kuweza kubeti usiku na mchana, na huku hauwezi kuchelewa kwani unaweza pia kubeti kwenye mchezo unaoutaka hata kama ukiwa live.
- Huduma bora kwa wateja
Tumejizatiti kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma za thamani muda wote na utofauti wa kipekee kucheza na parimatch, watoa huduma wetu wapo tayari kukuhudumia muda wote ndani ya masaa yote 24 kwa siku zote 7 za wiki iwe ni kwa e-mail, simu au kuchati, wao wapo kwa ajili yako.
Parimatch Inachakataje Odds za Double Chance?
Kama utakavyokua umeshagundua odds za Double chance ni ndogo zaidi ya odds za kawaida au tuseme ni ndogo kuliko odds za mikeka ya single, hii ni kwa sababu una nafasi mara mbili ya kushinda unapocheza Double chance, mchakato wa kupata odds za Double chance siyo mgumu kama watu wengi wanavoyfikiri.
Ili uweze kupata odds za kubeti kwa Double chance, unachukua odds za matokeo hayo mawili yakiwa tofauti kisha unazidisha, kisha unagawanya majibu ya kuzidisha kwa majibu ya kujumlisha namba hizo mbili.
Timu A kushinda au Kutoa sare = Odds za Timu A * Odds za Draw (Odds za Timu A + Odds za Draw)
Je, Kutakuwa na Faida Kuweka Mikeka Miwili Tofauti?
Kwanza kabisa lazima ujue hauwezi kuweka matokeo mawili tofauti kwenye tukio moja kwa kuwa huu utakuwa ni udanganyifu, ndiyo maana hakuna hili soko.
Licha ya hivyo hebu ngoja tufikirie mambo yangekuwaje kama hili lingeruhusiwa, tuchukulie mfano huu wa Norwich City vs Watford FC.
Mkeka wa 1×2
1 | 2.65 | Draw | 3.55 | 2 | 2.55 |
Mkeka wa Double chance
1 or Draw | 1.47 | No draw | 1.28 | 2 or Draw | 1.43 |
Odds za kwamba Norwich atashinda ni 2.65, na Watford kushinda ni 2.55, huku sare ikiwa na odds za 3.55, imagine umeweka dau la TZs 100,000, na huu ukawa mkeka wa timu moja tu, japo ukitaka kupunguza risk yako kwa kuweka matokeo mawili (Norwich kushinda au Kutoa sare) mkeka wa Double chance una faida sana.
Hebu fikiria kama unawabetia Norwich kushinda au Kutoa sare, unagawanya TZs 100,000 kwenye mikeka miwili ya TZs 50,000 kila mmoja Kushinda au Kutoa sare. Unaweka mkeka mmoja kwa Norwich kwa mkeka mmoja wa 2.65, na mkeka wa TZs 50,000 kwenye Draw kwa odds 3.55, tuseme Norwich wakitoa sare utashinda TZs 177,500. Japo kupata faida inakubidi utoe kiwango cha awali cha TZs 100,000 hii inakuacha na faida ya TZs 77,500.
Tuseme Norwich wakashinda kwa upande mwingine, utaishia kupata TZs 132,500. na kukuacha na faida ya TZs 32,500.
Sasa fikiria kuwa uliweka mkeka kwenye Double chance kwa Norwich kushinda au kutoa sare. Odds zako ni 1.47 na ukaweka TZs 100,000 kwenye matokeo haya. Hapa Norwich akishinda au akitoa sare utashinda faida ya TZs 47,000.
Kama unavyoona mwenye kubeti kwa Double chance kuna faida zaidi kusawazisha ulingo kwa timu ndogo, ili ujue kuwa utashinda kiasi gani lazima uwe muangalifu kwenye odds.
Double Chance Ni kwa Ajili ya Mafundi au Hata kwa Watu Wanaojifunza?
Double chance ndiyo mbinu rahisi zaidi ya kubetia na kushinda kwa kuwa unapata nafasi kubwa zaidi ya kushinda kwa kuwa una nafasi mara mbli ya kucheza na kushinda, kwa maana hii Double chance huwa inaonekana kama mbinu ya watu wanaojifunza, mara nyinyi mafundi wengi hawajisumbui kutafuta odds ndogo.
Mafundi wengi wanapenda kuchagua mechi nyingi kwa Double chance na kuweka dau kubwa sana ili waweze kuona faida, wataalamu wengi wa hizi kazi wanatumiaga Double chance kujaza odds kwenye mikeka yao.
Kubeti kwa Double chance kunaweza kuwa kwa faida yako, kujitahidi kubeti kwa timu ndogo ila unaweza kuweka Double chance ili kupunguza uwezekano wa kupoteza na kuongeza uwezekano wa kushinda mkeka wako.
Masoko Zaidi ya Kubashiri kwa Ajili Yako
- Mkeka wa Handicap Ni Nini?
- Ubashiri wa Asian Handicap Umefafanuliwa
- Moneyline Ni Nini katika Kubeti Michezo?
- Fahamu Mbinu za Kubashiri Matokeo ya 1×2
- Timu Zote Mbili Kufunga Katika Kubeti
- Kubetia Matokeo Sahihi: Yote Unayohitaji Kuyajua
- Mikeka ya Magoli Witiri/Shufwa Imeelezewa
- Mikakati ya Kubeti Halftime/Fulltime Imefafanuliwa
- Kubeti kwa Over/Under (Total) Kumeelezewa katika Maneno Rahisi
- Dondoo na Mbinu 3 za Juu za Kubeti kwa Over/Under
- Ufafanuzi wa Draw No Bet
- Kubeti Sare: Yote Unayohitaji Kuyajua
- Mkakati wa Kubeti Goli la Dakika za Lala Salama Umeelezewa
- Parlays na Teasers Ni Nini?
- Ufafanuzi wa Mikeka ya System
- Nini Maana ya Mkeka Wenye Mechi Nyingi?
- Mikeka ya Futures Imeelezewa katika Maneno Rahisi
- Aina za Mikeka ya Soka Zimeelezewa
Pata nafasi mara mbili ukiwa na Parimatch
Unasubiri nini? Sasa ambapo unajua kila kitu kinachohusiana na kucheza Double chance, kama bado unajiuliza kama kubeti kwa Double chance ni kwa ajili yako, jiulize kama unatosheka na kupata faida kidogo, kama unatosheka basi, hii ni ya kwako kabisa.
Double chance pia hutumika endapo unataka kuipa ushindi timu ndogo lakini unataka kupuguza uwezekano wa kupoteza hela zako na uwezekano mkubwa wa kushinda pia, vilevile kama una uwezo wa kuweka dau kubwa basi hii ni kwa ajili yako.
Pakua app ya Parimatch leo kupata fursa ya kufurahia kucheza kwenye mechi nyinyi za Double chance kwenye handball, soka na michezo mingine mingi mno! Usipitwe na fursa ya kubeti kwenye michuano mingi ya kukupa hela kwenye Double chance barani Afrika, jisajili leo!
Maswali ya Mara kwa Mara
Nini maana ya Double chance kwenye kubeti?
Double chance kwenye kubeti inarejelea dau la matokeo mawili kati ya matatu yanayoweza kutokea ya mechi ya michezo. Uwezekano wa Double chance una kiwango cha 66.6% kwenye utabiri. Utajua utabiri huu kupitia ishara za 1X, 2X, na 12.
Je, Double chance inafaa kwenye kubeti?
Double chance kwenye kubetia inaweza kuwa nzuri ikiwa unataka kushinda michezo kati ya timu mbili zilizo wazi. Kwa mfano, dau la Double chance kwa timu za nyumbani na ugenini huongeza nafasi zako za kushinda hasa timu zinapofunga mabao mengi lakini sare chache,
Je, Double chance 2x ina maana gani?
Double chance 2X inarejelea timu ya pili au mchezaji kushinda au sare. Hii inamaanisha kuwa wachezaji wanapata nafasi mbili za kushinda kwenye mkeka – nyumbani au ugenini. Kwa kawaida, matokeo ni ushindi wa timu ya nyumbani, ushindi wa timu ya ugenini au sare.