Wanacheza – Unashinda Jiunge sasa
Mwanzo / / Mikeka ya Magoli Witiri/Shufwa Imeelezewa

Kama unatafuta njia rahisi ya kuanza kubeti mtandaoni, magoli witiri (odd)/shufwa (even) ni chaguo rahisi sana la kubetia na la kukufanya uanze na uendelee kubashiri vyema. Na app ya kubetia michezo ya Parimatch ni jukwaa bora la kuanzia jambo hili. Timu yetu ya wataalamu wa teknolojia imeunda app hii ili iwe ni rahisi sana kadri inavyowezekana kuitumia. Ikiwa ndiyo mara yako ya kwanza au umechefuliwa na umechoshwa na app nyingine nyingi, umepata njia bora ya kuweka mikeka yako.

Kama unashangaa “witiri/shufwa” (“odd/even”) humaanisha nini katika kubetia, umekuja kwenye sehemu sahihi. Muongozo huu rahisi kutumia utakupitisha kwenye kila kitu unachohitaji kukijua wakati wa kuweka mikeka ya magoli witiri/shufwa. Muhtasari huu umeundwa ili kukusaidia kuelewa maana ya witiri/shufwa katika kubetia, wakati gani ni mzuri zaidi kuitumia mbinu hii, na jinsi ya kutengeneza faida pale inapowezekana. Pia, tutakupatia muhtasari wa faida na hasara za mikeka ya magoli witiri/shufwa.

Magoli Witiri/Shufwa (Odd/Even) ni Nini?

Kubetia magoli witiri/shufwa hurejelea kwenye mtindo wa kubeti ambapo wabashiri hubetia kwenye ikiwa idadi ya jumla ya magoli mwishoni mwa mchezo au mechi ni witiri au ni shufwa.

Kama wewe ni mpya kwenye kubeti mtandaoni au kucheza kamari ya michezo kwa ujumla, kamwe unaweza ukawa haujawahi kulisikia neno hili. Rahisi sana kuuelewa, mtindo huu wa kubeti ni mbinu nzuri kwa wabashiri wapya. Kama ungechukua mchezo wa soka, kwa mfano, mwisho wa dakika 90 kamili, alama za timu zote mbili zinajumlishwa pamoja. Kama hii ni sawia na namba witiri (1, 3, 5, na kadhalika), haya ni “Magoli Witiri”. Kama, kwa upande mwingine, idadi ya jumla ya magoli kutoka kwenye timu zote mbili katika mechi yote ina jumla ya namba shufwa (0, 2, 4, na kadhalika), haya yangekuwa ni “Magoli Shufwa”.

Fikiria mchezo wa soka kati ya Brighton Hove na Watford FC.

Kama Brighton ingeshinda mchezo kwa 2-1, hii ingemaanisha kuwa idadi ya jumla ya magoli kwenye muda kamili ingekuwa ni magoli matatu. Hii ni kwa sababu unajumlisha pamoja magoli mawili yaliyofungwa na Brighton na goli moja lililofungwa na Watford. Kama uliweka mikeka kwenye “Witiri”, ungeshinda hii mikeka kwa maana tatu ni namba witiri. Hata hivyo, ikiwa, Brighton ilishinda kwa 3-1 au timu hizi zilitoka sare ya 2-2, hii ingekuwa jumla ya magoli manne. Katika hali hii, ungepoteza hii mikeka kwa maana magoli manne yangekuwa ni namba shufwa ya magoli.

Wabashiri wengi hupendelea kuweka mikeka ya witiri/shufwa kwa sababu humfanya mbashiri ajishughulishe kwenye mchezo mzima, tofauti na aina nyingine za kubetia kama vile overs/unders. Fikiria kuwa umeweka mikeka ya over/under (totals) kwa chini ya magoli 2.5 na goli la tatu linafungwa. Kwa kuvunjwa moyo kutoka kwenye mikeka yako iliyopotea, una uwezekano wa kutokujishughulisha na mchezo. Kwenye mikeka ya magoli witiri/shufwa, unahusishwa hadi mwisho kabisa wa mechi, kwa maana unategemea kwenye alama ya mwisho kabisa kujua ikiwa umeshinda au umepoteza.

“Magoli Witiri” Humaanisha Nini?

Kama ilivyoelezwa hapo juu, lengo la mikeka ya shufwa/witiri ni kujaribu na kuamua ikiwa idadi ya mwisho ya jumla ya magoli au alama itaendana na namba witiri au shufwa. Pindi ukiweka mikeka kwenye “Magoli Witiri”, unatabiria kuwa mchezo utamalizika kukiwa na jumla ya alama iliyojumlishwa ambayo ni namba witiri.

Kama ukifikiria kuhusu hili, papo hapo huondoa nafasi ya sare kutokea. Kwa kubetia kwenye “Witiri”, unabetia kuwa hufikirii kungekuwa na uwezekano wa sare. Hiki ni kitu cha kufikiria kabla ya kuweka mikeka kama hiyo. Hii ni kweli hasa kama unabeti kwenye michezo ya soka kwa maana 25% kati ya michezo yote ya ligi kuu ndani ya miaka 12 iliyopita iliishia kwa matokeo ya sare.

Unaweza ukawa unafikiria kuwa ungeweza kulirudisha hili nyuma kwa muda kidogo wa ziada. Kwa mfano, kama ungebeti kwenye mchezo wa kikombe wenye mzunguko wa mtoano badala ya mchezo wa ligi, kungekuwa na muda wa ziada au mikwaju ya adhabu kuamua mshindi, kwa maana hapataweza kuwa na sare. Wakati hili linaweza kuwa ndiyo suala lako, mikeka ya witiri/shufwa huzingatia tu magoli yaliyofungwa ndani ya dakika 90 kamili. Muda wa ziada na mikwaju ya adhabu havihusishwi. Hii humaanisha kuwa kama mechi inamalizika kwenye 2-2 na mikwaju ya adhabu inaamua mshindi, mikeka yako itatumika tu kwenye 2-2 hivyo ungepoteza mikeka ya “Magoli Witiri”. Muda wa majeruhi unahusishwa, hata hivyo, ni kwa sababu muda huu huwepo kufidia muda uliopotezwa mapema zaidi katika mchezo wa dakika 90.

Ingawa, kwa kifupi, inapokuja kwenye maana ya magoli witiri, aina hii ya mikeka hushinda kama jumla ya idadi ya magoli yaliyofungwa na pande zote mbili ni sawa na namba witiri kwenye muda kamili.

“Magoli Shufwa” Humaanisha Nini?

“Magoli Shufwa” yanaweza kufikiriwa kama kinyume cha “Magoli Witiri”. Pindi ukiweka mikeka “Shufwa”, unabetia kuwa idadi ya jumla ya magoli yaliyofungwa na pande zote mbili ni namba shufwa kwenye muda kamili.

Kama tu “Magoli Witiri”, hii haihusishi muda wa ziada au mikwaju ya adhabu — siyo kuwa matokeo hayo yangekuwa yanahusika hapa. Ingawa kinachovutia, mikeka ya “Magoli Shufwa” hukulinda kutoka kwenye sare. Kama wabashiri wazoefu wanavyojua, mikeka za 1X2 inaweza kuwa haitabiriki kwa maana sare huchezesha matokeo na odds. Kama ilivyoelezewa hapo juu, sare hutokea katika soka 25% ya muda wote. Hii ni takwimu kubwa kuipuuza. Pindi ukibetia kwenye “Magoli shufwa”, hata hivyo, una sare kwenye upande wako kwa maana sare daima ni namba shufwa.

Kwa kufupisha, mikeka ya “Magoli shufwa” inaweza kuelezewa kama mikeka ambapo unabashiri kuwa idadi ya jumla ya magoli mwishoni mwa mechi itakuwa sawa na namba shufwa.

0-0 Ni Witiri au Shufwa katika Kubeti?

0:0 (bila bila) kama matokeo ya mchezo ni matokeo shufwa. Katika mahesabu, sifuri ni namba shufwa, lakini hata haijalishi. Mchezo uliomalizika katika sare utapelekea kwenye jumla ya namba mbili zinazofanana ambazo daima zitakuwa ni namba shufwa.

Je, Nibeti kwenye Magoli Witiri au Magoli Shufwa?

Kwa ujumla, utaona ya kuwa mameneja ubashiri wana tabia ya kufanya odds kiasi fulani ziwe sawa kwa matokeo yote mawili, shufwa na witiri. Kutokea mwanzo, inaweza kufikirika kama una nafasi ya 50/50 ya matokeo kuwa aidha shufwa au witiri, lakini ukichimba chini kidogo, unaona hii mara zote siyo suala halisi. Hii inaweza kutegemea kwenye wastani wa idadi ya magoli ambayo yanafungwa kwenye mchezo.

Hebu tuchukulie soka, wa mfano. Kama chati hapo chini inavyoonesha, nafasi za mchezo wa soka kwenda juu ya jumla ya magoli 6 ni ndogo sana. Kwa kuzingatia kuwa 0 ni namba shufwa katika magoli witiri/shufwa, matokeo husogezwa kuelekea shufwa (kutokana na matokeo ya bila bila).

Mzunguko wa Matokeo ya Soka

Chanzo: FiveThirtyEight

Kwa mikeka ya “Magoli Shufwa” kulipa, matokeo ya mwisho yanawezekana kuwa moja ya alama zifuatazo:

0-0, 1-1, 1-3, 1-5, 2-0, 0-2, 2-2, 2-4, 3-1, 3-3, 4-0, 0-4, 4-2, 5-1, 6-0, 0-6

Kwa mikeka ya “Magoli Witiri” kulipa, matokeo ya mwisho yanawezekana kuwa moja ya alama zifuatazo:

1-0, 0-1, 0-5, 1-2, 1-4, 2-1, 2-3, 3-0, 3-2, 4-1

Kutokana na kwamba zaidi ya magoli sita ni nadra sana katika mchezo, matokeo huchezeshwa kidogo kuelekea “Magoli Shufwa” kwa maana 0-0 na jumla ya magoli 6 yote mawili huhesabika kuwa ni shufwa.

Masoko Gani ya Kubetia ya Witiri/Shufwa Yanapatikana Parimatch?

App ya Parimatch ya kubetia michezo hutoa mikeka ya witiri/shufwa iliyo rahisi zaidi. Wakati wabashiri wanaweza kuweka mikeka witiri/shufwa kwenye muda kamili wa mechi au mchezo, pia tuna utajiri wa masoko mengine yanayohusiana nayo kuunogesha mchezo kwa ajili yako.

Kwa mfano, inapokuja kwenye kubeti mpira wa miguu, magoli witiri/shufwa yanaweza kugawanywa katika vipindi vyote viwili. Humaanisha, kwenye Parimatch, wabashiri wanaweza kufurahia kuweka mikeka kwenye witiri/shufwa katika kipindi cha kwanza, katika kipindi cha pili au katika vipindi vyote viwili. Si hilo tu, watumiaji wanaweza pia kufurahia kuweka mikeka ya magoli witiri/shufwa kwenye kila timu pekee yake.

Katika michezo mingine, mikeka kama hiyo ni tofauti zaidi. Katika mpira wa wavu, kwa mfano, Parimatch huwawezesha wabashiri kubetia kwenye witiri na shufwa kwa seti mojamoja.

Kitu kingine kizuri kuhusu app ya Parimatch, ni kuwa huwapa watumiaji wetu wote masoko ya “Magoli Witiri/Shufwa” katika aina tofauti ya michezo. Wabashiri wanaweza kuweka mikeka witiri/shufwa kwenye soka, mpira wa kikapu, mpira wa magongo kwenye barafu, mpira wa wavu, raga, na zaidi. Pamoja na mkusanyiko mpana kama huo wa michezo iliyopo, haishangazi kuwa Parimatch hujulikana kama app bora ya kubeti michezo barani Afrika!

Jinsi ya Kubetia Magoli Witiri/Shufwa Ukiwa na Parimatch

App ya Parimatch ya kubetia michezo imeundwa kwa urahisi wa kutumia akilini mwake. Ni kitu bora kwa wabashiri wanaoanza na wacheza kamari wazoefu vilevile, app ya Parimatch ina dashibodi angavu, kuifanya iwe ni rahisi sana kuipitia. Iliyo haraka, yenye nguvu, na ya kuaminika, app ya Parimatch hukupa upatikanaji wa mkusanyiko mpana zaidi wa machaguo ya kubetia mtandaoni barani Afrika, moja kwa moja kutoka kwenye vidole vyako.

Download the Parimatch app

Kwa urahisi, fuata maelekezo haya ya haraka ili kukuelekeza juu ya kuweka mikeka ya witiri/shufwa:

  1. Ingia kwenye akaunti yako ya Parimatch na hakikisha umeweka pesa;
  2. Chagua kubetia “Mchezo”, “Live”, au “Virtual” kutoka kwenye menyu ya chini yake;
  3. Bofya kwenye mchezo ambao ungependa kuuwekea mikeka;
  4. Chagua nchi ambapo mechi hiyo inachezwa;
  5. Chagua ligi au shindano unalohitaji;
  6. Bofya kwenye mchezo unaoubetia;
  7. Nenda chini kutafuta “Witiri/Shufwa” na chagua aidha Witiri au Shufwa;
  8. Nenda kwenye tiketi ya ubashiri kumalizia mikeka yako.

Faida na Hasara za Mikeka ya Magoli Witiri/Shufwa

Kubetia witiri/shufwa ni sehemu nzuri ya kuanzia kama wewe ni mbashiri unayeanza kazi. Ni rahisi kuelewa na una nafasi nzuri sana za kushinda. Hata hivyo, kuna mambo machache ya kuyaweka akilini.

Faida za Mikeka ya Magoli Witiri/Shufwa

  • Mikeka bora ya anayeanza kujihusisha na kubetia

Kubetia witiri/shufwa ni furaha nzuri kwa maana ni rahisi kuelewa na una nafasi kubwa kiasi fulani ya kushinda — matokeo yatakuwa ni aidha shufwa au witiri! Kwa maana hii, inaweza kuwa inafurahisha kidogo kama hutaki kuziangalia takwimu na unataka kukisia tu. Mara nyingi zaidi, odds huwa zinasawazishwa vizuri kwa njia yoyote.

  • Nafasi kubwa sana ya kushinda

Odds za kubetia witiri/shufwa kwa kawaida ni sawia tu kwa jibu lolote. Hii ni kwa sababu una takribani nafasi ya 50/50 ya kupata hili kwa usahihi, hata kama ukizisoma takwimu. 50% ni nafasi kubwa sana kuibetia.

  • Mikeka ya shufwa hukulinda dhidi ya sare

Kama wabashiri wazoefu wanavyojua, sare inaweza kuchezesha tabiri zako za kubetia, hasa kwenye mikeka ya mshindi (1X2). Kama tulivyosema kabla, sare hutokea 25% ya muda wote katika soka, hivyo ni muhimu kulizingatia hili wakati wa kubetia. Mikeka ya shufwa/witiri haizingatii muda wa ziada au mikwaju ya adhabu, ikimaanisha sare daima inawezekana. Zaidi ya hilo, sare daima ni shufwa. Kwa maana hii, kubetia kwenye idadi shufwa ya jumla ya magoli inaweza kuwa ni faida kwenye kulinda zaidi dau lako.

Hasara za Kubetia Witiri/Shufwa

  • Matokeo ya odds ndogo katika ushindi mdogo

Kutokana na kwamba kuna karibia nafasi ya 50/50 ya wewe kushinda mikeka shufwa/witiri, odds hizi huwa ndogo sana. Kwa maana hii, kiukweli hautatengeneza faida kubwa kutoka kwenye odds za jumla na kubetia Shufwa.

  • Siyo nzuri kwa mikeka ya parlay

Kama unapenda kuweka mbinu kwa kutumia parlay wa kubeti, unaweza kukuta kuwa mikeka ya witiri/shufwa haileti matokeo yanayohitajika yenye faida. Hii ni kwa sababu odds hizi ni nadra kuwa juu ya 2.00, hivyo ni ngumu kurudisha dau lako kama moja ya tabiri zako katika parlay haitakulipa.

Je, Ubetie Magoli Witiri au Shufwa?

Hili ni swali zuri na jibu hutegemea kwenye nini unatumai kukipata kutoka kwenye mikeka yako. Kama wewe ni mcheza kamari mzoefu unayetafuta kutengeneza pesa nyingi kwa kuziwekea mbinu za mikeka, mikeka ya witiri/shufwa inawezekana siyo kitu cha kuvutia kwako. Siyo yenye kukufaa kiukweli kwa mikeka ya system, odds ndogo hazileti mapato makubwa, hata kama ukishinda.

Kwa upande mwingine, kama unatafuta kuweka mikeka kwa ajili ya kufurahia kidogo, hii ni mikeka mizuri. Ina nafasi kubwa ya kushinda — karibia 50% kwa kila upande. Wakati odds ni ndogo, hii huonesha tu nafasi za kushinda ni kubwa kwa kiwango gani. Kwa maana hii, inaweza kuwa ni faida nzuri na ndogo kwa mteja anayebashiri upya, kupata furaha kidogo.

Sawa na hilo, kama unatafuta mikeka ambayo itakufanya ujishughulishe katika mchezo mzima, kubetia witiri/shufwa kwa jumla ni njia nzuri sana ya kusisimua ukiwa na mechi nzima kwa maana unatakiwa kusubiria mpaka mwisho kabisa kujua kama mikeka yako imekulipa. Tofauti na kubetia kwenye overs/unders, ambapo unaweza kujua ikiwa mikeka yako imekulipa kwenye pointi yoyote katika mchezo, witiri/shufwa humaanisha unahitaji kuangalia mpaka mwisho kabisa.

Unaweza Kutengeneza Faida kwa Kubetia kwenye Magoli Witiri au Shufwa?

Kama ilivyo kwenye mbinu yoyote ya kubeti, kuna faida inayotakiwa kulipwa kama ukishinda mikeka. Hata hivyo, kubetia witiri/shufwa kuna uwezekano mkubwa wa kukulipa wewe, haijalishi ni chaguo gani unalolichagua. Wakati takwimu na chambuzi zinapohusika, kuna takriban nafasi ya 50/50 kwamba aina hii ya mikeka itafanya kazi kwako na kutoa faida kidogo.

Pamoja na hili akilini, kwa maana nafasi za kushinda hii mikeka ni kubwa sana, mara nyingi dau lake ni dogo sana. Hii humaanisha kuwa utaona kwa nadra dau juu ya 2.00 pindi ukibetia kwenye witiri/shufwa kwenye mchezo mzima. Kwa maana hii, wakati mikeka iliyoshinda itakapolipwa, haitalipwa kiasi kikubwa sana.

Hilo likiwa limeshasemwa, dondoo moja ni kubetia kwenye magoli ya kipindi cha kwanza. Utakuwa unakuta odds kubwa zaidi katika kubetia witiri/shufwa kwenye kipindi cha kwanza kwa maana mameneja ubashiri hukuta ni rahisi zaidi kutabiri ikiwa timu itafunga katika kipindi cha kwanza kutegemeana na historia yao ya uchezaji.

Mazingira mengine ambapo unaweza kutengeneza faida kubwa zaidi kwenye kubeti shufwa/witiri ni wakati ukibetia kwenye timu dhaifu. Kama ni dhahiri kuna timu pendwa, unaweza kukuta kuwa aina hii ya odds kwa timu dhaifu ni ndogo zaidi kwenye chaguo la Shufwa. Hii ni kwa sababu meneja ubashiri hafikirii kama timu dhaifu itafunga kabisa. Katika suala kama hili, mikeka ya “Witiri” huwa na odds kubwa zaidi. Katika hali ambayo timu dhaifu inaweza kufunga goli, ungeweza kushinda faida kubwa sana.

Mbinu nyingine ambayo wabashiri baadhi huitumia kuongeza mapato yao kutoka kwenye kubetia witiri/shufwa, ni kwa kutumia mifumo ya muendelezo. Hili linafanyika kwa kusubiria mpaka mechi ya tatu ya msimu na halafu kuchagua timu ambazo zote zimemaliza michezo yao na jumla zao ni witiri. Halafu unaweka mikeka kwenye mechi inayofuata kumalizika kama jumla shufwa. Kama mikeka hii haikulipi, ongeza dau lako kwenye mikeka inayofuata kwa 2.2. Kwa maana hii, kama dau lako la kwanza lilikuwa ni TZs 300, dau lako la pili lingekuwa TZs 660. Kama mikeka inayofuata hailipi, unaongeza dau kwa 4.4, hadi TZs 2904. Wazo ni kwamba mikeka yako mwishowe itakulipa, na itakulipa kufidia madau yote yaliyopotea kabla. Wakati hili linaweza kufanya kazi, mifumo ya kubeti kwa muendelezo ni yenye hatari sana na inaweza kumaliza salio lako la benki kwa ajili ya kubetia haraka sana. Usiziruhusu aina hizi za mikeka kuwa ngumu kuzizidhibiti, kwa maana unaweza kupoteza kiwango kikubwa haraka sana kama unakuwa haupo sahihi kwenye mizunguko michache!

Kipi Kingine Unachoweza Kukibetia Uwapo na Parimatch?

Utofauti wa aina za mikeka kwenye Parimatch ni mkubwa kiukweli. Hii hapa ni sehemu tu ya masoko ya mikeka yaliyopo:

Muhtasari wa Magoli Witiri/Shufwa

“Magoli Witiri/Shufwa” ni mbinu rahisi sana ya kubetia. Imeundwa zaidi kwa ajili ya furaha kidogo kuliko kuwa mpango wa kutengeneza faida, wabashiri wanaoanza na wasio wa kulipwa wanaweza kufurahia mikeka hii iliyo rahisi kuiweka. Ikiwa na nafasi ya takriban 50/50 ya mafanikio, wabashiri wana uwezekano mkubwa wa aina hii ya mikeka yao kulipa. Hata hivyo, kutokana na kwamba mikeka ya witiri/shufwa ina nafasi kubwa kiasi fulani, odds ni ndogo, hivyo ukingo wa faida ni finyu.

Kutokana na kwamba odds zinacheza pande zote mbili, wacheza kamari wengi wazoefu watakuambia kuwa aina hii ya kubeti ni kazi ya kukisia tu. Kusoma takwimu kiukweli hakutasaidia kuboresha nafasi zako za kushinda. Hilo likiwa limesemwa, kama unataka kutumia mfumo wa kubeti kwa muendelezo kuongeza nafasi zako za kutengeneza faida kubwa zaidi, basi utahitaji kuzingatia matokeo ya michezo ya karibuni ya timu. Ingawa, ni muhimu kutambua hatari za mifumo ya kubeti kwa muendelezo.

Kwa kifupi, Parimatch hufanya kuwezekana kuweka bashiri za witiri/shufwa tofauti kwenye app yetu ya kubetia michezo mtandaoni. Ni ya haraka kuipakua na ni rahisi kuitumia, app yetu huangazia mikeka witiri/shufwa kwa aina zote za michezo, kutoka mpira wa kikapu hadi mpira wa wavu, kutoka soka hadi raga. Unaweza kuweka mikeka kama hiyo kwenye mchezo mzima, kila kipindi pekee yake, na kila timu inapocheza.

Usipoteze muda! Jaribu bahati yako leo!

Maswali ya Mara kwa Mara

Kuna utofauti gani kati ya magoli witiri na magoli shufwa?

Magoli witiri yana jumla ya namba isiyo ya kawaida, yaani, 1, 3, 5, 7, na kadhalika. Magoli shufwa yana jumla ya namba shufwa, yaani, 2, 4, 6, 8, na kadhalika. Mara nyingi magoli shufwa na witiri hutumiwa na wale wanaobetia kwenye mchezo au kubeti mtandaoni.

Je, shufwa na witiri zinamaanisha nini?

Witiri inamaanisha kwamba mteja anatabiri kuwa mchezo utaisha kwa mchanganyiko wa jumla wa alama katika namba isiyo ya kawaida, kama vile 1, 3, 5, 7, 9, na kadhalika. Shufwa inamaanisha kuwa mdau anatabiri kuwa mchezo utaisha kwa jumla yenye mchanganyiko wa alama katika namba ambayo ni sawia, yaani, 2, 4, 6, 8, 10, na kadhalika.

Ni nini witiri au shufwa kwenye kubashiri? (Even/odd)

Kwenye kubashiri, shufwa na witiri hurejelea uainishaji wa matokeo au takwimu mahsusi katika tukio la michezo. Inatumika sana kwenye masoko kama vile mkeka wa magoli pungufu au zaidi ya. “Odd” huonesha matokeo au takwimu inayosababisha namba witiri, ilhali “even” inaonesha matokeo au takwimu inayosababisha namba shufwa. Uainishaji unategemea jumla ya takwimu au matokeo husika.

Je, shufwa kwenye dau inamaanisha nini?

Shufwa kwenye dau ni pale mdau anapoweka dau kwamba mchezo anaoubetia utaishia na mchanganyiko wa alama zilizo katika idadi sawa, kama vile 2, 4, 6, 8, 10, na kadhalika. Hii ina maana kwamba wewe unatabiri kuwa hakuna nafasi kwamba jumla ya alama itaishia kwenye witiri au sare.

Je, 0-0 ni shufwa au witiri kwenye kubashiri?

Kwenye miktadha mingi ya kamari, alama ya 0-0 inachukuliwa kuwa ni sawa. Kwa upande wa masoko ya kubashiri ambayo yanahusisha namba zisizo za shufwa ama za witiri, kama vile miekka ya magoli zaidi ya au pungufu ya au jumla ya mikeka ya magoli, kwa kawaida matokeo ya 0-0 yanaweza kuainishwa kama matokeo sawia. Hata hivyo, daima ni muhimu kurejelea sheria na masharti mahsusi ya soko la kubeti au kampuni unayotumia, kwa kuwa kunaweza kuwa na tofauti za jinsi zinavyoainisha na kusuluhisha matokeo kama hayo.

Je, sifuri ni namba witiri ama namba shufwa kwenye kubashiri?

Kwenye miktadha mingi ya kubeti, sifuri inachukuliwa kuwa namba shufwa. Linapokuja suala la soko la kawaida/hata la kubashiri, ambapo unatabiri kama matokeo au takwimu mahsusi itakuwa ni yenye namba shufwa ama namba witiri, kwa kawaida sifuri huainishwa kama namba shufwa. Hata hivyo, ni muhimu daima kukagua sheria na masharti mahsusi ya soko la kubeti ambalo unalitumia.

Je, unahitaji kuwa wa kwanza kupata taarifa mbalimbali?

Subscription was successfully completed.