Mikeka ya total au over/under ni aina maarufu ya mikeka ambapo hauhitaji kukisia mshindi. Unatabiri tu idadi ya magoli katika mechi ya mpira wa miguu, mizunguko katika pigano la UFC, michezo katika mechi ya tenisi, n.k. Cha zaidi, haubeti kwenye idadi halisi — unakisia tu ikiwa namba ni kubwa zaidi (over) au ndogo zaidi (under) kuliko namba iliyopangwa na meneja ubashiri.
Tunaelezea yote hayo kwa kina katika mwongozo wetu wa kubeti kwa totals. Hata hivyo, ikiwa tayari umelielewa wazo la jumla, ni muda wa kuingia kwa undani zaidi. Kama unataka kupata kilicho bora kutoka kwenye kubeti kwa over/under, tuna dondoo na mbinu chache za ndani kwa ajili yako.
Yaliyomo
Weka Ulinzi Akilini
Hebu kwa haraka tujikumbushie machaguo ya kubeti kwa totals. Unaweza kubeti kwenye overs kutabiri kuwa tukio fulani (kama vile magoli yaliyofungwa) yatatokea mara nyingi zaidi kuliko meneja ubashiri anavyopendekeza. Badala yake, unaweza kubeti kwenye unders kama unaamini kitu fulani kitatokea mara chache zaidi kuliko kinavyopendekezwa.
Wakati wabashiri wengi hupendelea kubeti kwenye overs, wakitumaini kuipa nguvu timu kupata alama, hii sio mara zote njia bora ya kutumia kubeti kwa totals. Aina hii ya kubeti kwa totals hulenga kwenye ushambulizi wa timu na mara nyingi hutumika wakati timu yenye nguvu inapokutana na timu dhaifu.
Wakati kwa kulenga kwenye ushambulizi kutakusaidia kuelewa jinsi wachezaji na timu zilivyo makini kufunga alama, unaweza ukawa unakadiria kwa upungufu umuhimu wa safu ya ulinzi. Kubeti kwenye overs kunaweza kuonekana kama mpango usioweza kushindwa kama unafikiri timu yako inakwenda kuwa mfungaji wa juu, lakini kwa kuielewa safu ya ulinzi ya timu kutakusaidia kujua kwenye kiwango gani magoli au alama hizo zinaweza kuongezwa.
Pindi ukiifikiria safu ya ulinzi, usiangalie tu kwenye jinsi timu moja inavyojilinda dhidi ya nyingine. Hakika, unaweza kuwa na timu mbili zinazojilinda sana na hii inaweza kuonekana kama itaweka ufungaji wa magoli chini, lakini nani anamlinda nani kwenye kiwango cha mtu binafsi?
Mchukulie Willy Boly au Conor Coady wa Wolverhampton Wanderers. Wachezaji wote hawa wawili ni walinzi wenye nguvu sana na watasaidia kuziweka alama chini kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, tuseme kuwa Boly anamkaba Jamie Vardy wa Leicester City — mfungaji bora katika Ligi Kuu. Wakati Boly ni mzuri, Vardy ni mzuri zaidi, ambacho kwa kiasi fulani kinatangua alama ya Boly ya ulinzi. Kwa maana hii, labda wakati wa kubeti kwenye unders, unahitaji kuweka idadi yako juu zaidi.
Mbinu ambapo unazingatia safu ya ulinzi ya kila timu inaitwa mikeka ya handicapping totals. Mbinu hii ni bora inapotumika wakati una timu mbili zenye nguvu sana ambazo zina safu nzuri za ulinzi. Katika suala hili unabeti kuwa idadi ya jumla ya alama au magoli itakuwa chini ya namba fulani. Kwa kubeti kuwa alama zitakuwa chini ya, kimsingi unaipunguza alama. Kwa mfano, tuseme kuwa unaibetia mechi ya mpira wa miguu itamalizika kwa magoli yasiyozidi matatu, ungekuwa chini ya 3.5. Hii humaanisha unaipunguza jumla iliyopangwa hadi kwenye magoli yasiyozidi matatu.
Kuna mbinu kadhaa za kufahamu idadi ya juu ya magoli ambayo yana uwezekano wa kupatikana katika mchezo lakini uhitaji kusoma kidogo. Hii ndio njia maarufu hasa ya kubeti wakati wa kubashiri kwenye mpira wa miguu na mpira wa kikapu wa Kimarekani. Dondoo bora kwa ajili ya ku handicap ni:
- Angalia jinsi safu ya ulinzi ya kila timu ilivyo thabiti. Kama timu mbili zina safu nzuri ya ulinzi, magoli inawezekana yatakuwa chini. Kama timu moja ina safu dhaifu ya ulinzi, ni ngumu zaidi kukisia magoli mangapi yanaweza kuruhusiwa.
- Fikiria majeraha kwenye timu. Kama mchezaji mlinzi amejeruhiwa au kama mchezaji mbadala amechezeshwa, magoli mengi zaidi yana uwezekano wa kuruhusiwa. Hata hivyo, kama mshambuliaji muhimu amejeruhiwa au hachezi, ni rahisi zaidi kupunguza idadi ya alama.
- Je! Timu iko kwenye muda wa lala salama? Tazama kwenye historia ya nyuma ya timu. Timu baadhi zitajitanguliza mbele vizuri na halafu zitarudi nyuma kulinda kumalizia mchezo. Kama unabeti kwenye moja ya timu hizi, jaribu kutafuta utofauti gani wa magoli wataangukia nyuma. Inawezekana pindi wakiwa na uongozi wa magoli mawili, wanarudi nyuma. Hii itakusaidia kufahamu nani huweka alama chini na kwa kiasi gani wataitunza.
- Zingatia hamasa ya msingi ya timu. Kama kuna upinzani wa muda mrefu kati ya timu mbili zinazojilinda sana, una uwezekano wa kuwa na ufungaji wa chini.
Fikiria Kuhusu Hali ya Hewa
Katika mpira wa miguu wa Kimarekani, pepo zenye nguvu zinaweza kusababisha upungufu wa alama 2-3 katika mchezo. Sawia, katika soka, mapungufu ya ghafla ya halijoto yanaweza kusababisha shinikizo la mpira kupungua, kuufanya mpira kuwa bapa kidogo. Zaidi ya hilo, katika michezo yote miwili, mvua ya ghafla huathiri ubora wa kiwanja, kubadili uchezaji wa mchezo.
Ni muhimu kuelewa kuwa hali ya hewa iliyotabiriwa uhusishwa katika odds za matokeo ya mchezo. Hata hivyo, mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa hayahusishwi. Hii ni ya muhimu hasa wakati wa kubeti kwa overs na unders, haswa kama unabeti mubashara katika mchezo. Mvua ya ghafla au upepo uliyoongezeka vinaweza kupunguza idadi ya magoli au alama ambazo zinaweza kufungwa. Wekeza kwenye hili kama hali ya hewa inabadilika ghafla, kubeti kwenye unders za chini zaidi.
Mjue Kocha
Namna kocha au meneja anavyoitendea haki nafasi yake ni muhimu sana kwenye overs na unders hasa kama kuna kutokuendana kati ya uwezo wa timu. Kwa mfano, Manchester United kihistoria ni shambulizi, na Ole Gunnar Solskjaer akitunza utamaduni huo. Katika moja ya mechi zao dhidi ya Tranmere Rovers ambapo Manchester United walishinda 6-0, wangeweza kufunga kwa urahisi magoli 3 na kurudi nyuma kulinda kwa muda wote wa mechi uliyobakia. Hata hivyo, hivyo sivyo kocha wao anavyoichezesha timu. Kwa maana hii, kwa kumjua kocha na mipango yake kwa timu hukusaidia kujua ikiwa mchezo utakuwa wa ufungaji wa juu au chini kwa jinsi kocha anavyopenda kuwachezesha kwa ushambulizi au ulinzi.
Kwa usawia, fikiria kuhusu mashindano wanayocheza. Kama kocha analenga kwenye shindano moja zaidi ya lingine, atachezesha vikosi tofauti. Tuseme, kwa mfano, kuwa kocha wa timu ya soka analenga kwenye Ligi Kuu badala ya Kombe la FA, wanaweza kucheza kikosi dhaifu zaidi katika Kombe la FA. Hii inaweza kupelekea kwenye alama za chini zaidi katika michezo hii.
Masoko Zaidi ya Kubashiri kwa Ajili Yako
- Mkeka wa Handicap Ni Nini?
- Ubashiri wa Asian Handicap Umefafanuliwa
- Kubeti Kwa Double Chance Betting Ni Nini?
- Moneyline Ni Nini katika Kubeti Michezo?
- Fahamu Mbinu za Kubashiri Matokeo ya 1×2
- Timu Zote Mbili Kufunga Katika Kubeti
- Kubetia Matokeo Sahihi: Yote Unayohitaji Kuyajua
- Mikeka ya Magoli Witiri/Shufwa Imeelezewa
- Mikakati ya Kubeti Halftime/Fulltime Imefafanuliwa
- Kubeti kwa Over/Under (Total) Kumeelezewa katika Maneno Rahisi
- Ufafanuzi wa Draw No Bet
- Kubeti Sare: Yote Unayohitaji Kuyajua
- Mkakati wa Kubeti Goli la Dakika za Lala Salama Umeelezewa
- Parlays na Teasers Ni Nini?
- Ufafanuzi wa Mikeka ya System
- Nini Maana ya Mkeka Wenye Mechi Nyingi?
- Mikeka ya Futures Imeelezewa katika Maneno Rahisi
- Aina za Mikeka ya Soka Zimeelezewa
Muhtasari
Sasa kwamba unajua nini cha kuangalia katika mikeka yako ya total, ni muda kwa ajili ya mazoezi kiasi. Kama app bora ya kubeti michezo mtandaoni Africa, Parimatch inajivunia kutoa mkusanyiko mpana zaidi wa mikeka ya over/under kwa wateja wetu.
Si tu tunawapa watumiaji wetu michezo mingi ya kuchagua inapokuja kwenye kubeti kwa over/under, pia tumetengeneza app ya kubeti ya simu ya mkononi rafiki sana kwa mtumiaji na kiolesura rahisi kutumia, hisivu kwa ajili ya uzoefu wa kubeti usio na shida.
FAQ
Ni nini maana ya over na under?
Over na under ni aina ya kubeti ambapo unatabiri jumla ya mabao yatakayofungwa katika mechi kuwa juu (over) au chini (under) ya kiwango kilichowekwa na bookmaker.
Ni mfano upi wa over na under?
Mfano wa over na under ni kama bookmaker anaweka kiwango cha mabao kuwa 2.5. Kama unabeti ‘over’, unatarajia jumla ya mabao kuwa 3 au zaidi. Kama unabeti ‘under’, unatarajia jumla ya mabao kuwa 2 au chini.
Ni nini maana ya over under 2.5 mabao?
Over under 2.5 mabao inamaanisha kubeti kama jumla ya mabao katika mechi itakuwa juu ya 2.5 (yaani 3 mabao au zaidi) au chini ya 2.5 (yaani 2 mabao au chini).
Ni nini maana ya 1X2 over na under?
1X2 inawakilisha matokeo ya mechi: 1 (nyumbani anashinda), X (sare), au 2 (ugenini anashinda). Wakati wa kuchanganya na over/under, unatabiri matokeo ya mechi pamoja na jumla ya mabao yatakayofungwa.